Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemery Senyamule amefanya ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya wilaya ya kondoa leo tarehe 06/10/2022 kama zilivo ziara nyingine ndani ya mkoa ,katika ziara hii mkuu wa mkoa aliambatana na katibu tawala wa mkoa Dr Fatuma Mganga lakini pia kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na timu ya wataalam kutoka sekta mbali mbali mkoani na wataalam kutoka taasisi mbali mbali za serikali ikiwemo TANESCO ,RUWASA,TANROADS ,ARDHI NA TARURA.
Mh,Mkuu wa Mkoa aliwasili makao makuu ya Halmashauri yaliyoko katika kijiji cha Bukulu kilichopo kata ya Soera majira ya saa nne asubuhi na kupokelewa na watumishi wa halmashauri wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Dr.Makanachi, Mkurugenzi wa Halmashauri ndugu Mustapha Semwaiko Yussuf na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh,Abdallah Maguo.Mara baada ya kuwasili mgeni rasmi alipokea taarifa ya utekelezaji miradi mbali mbali inayotekelezwa na Halmashuri ikiwemo ujenzi wa jengo jipya la makao makuu ya halmashauri lenye thamani ya bil.3 ambalo tayari limefikia asilimia 70 na tayari limeanaza kutumika upande mmoja kwenye safu ya chini. Lakini pia taarifa ya utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya akina mama ,vijana na watu wenye ulemavu ambapo tayari Halmashauri ilikua imetenga fedha kama inavotakiwa kwa asilimia 100 pia taarifa ya mapato, Mkurugenzi alisema kwa kipindi hiki cha robo ya kwanza tayari Halmashauri imekusanya mapato kwa asilimia 25 kitu ambacho Mh, Mkuu wa Mkoa alipongeza kwa jitihada hizo pamoja na kua na vyanzo vichache sana vya mapato.
Baada ya kupata taarifa ya Halmashauri mgeni rasmi alipata fursa ya kuongea na Watumishi pamoja na Waheshimiwa madiwani wakati ambapo kila mmoja alipata wasaa wa kutoa kero yake na miongoni mwa maswali yalioulizwa ilikua ni pamoja na usumbufu wanaopata wananchi wa kijiji cha Hurui kutokana na kutokuwepo kwa daraja katika mto Hurui lakini pia ujenzi wa daraja katika mto Bubu kutokana na adha wanayoipata wananchi wa kata ya Serya,Changaa,Hondomairo na Thawi , Swali ambalo lilijibiwa na Meneja wa Tanroad Mkoa Eng.
Salehe Juma kua daraja la mto Hurui tayari mkandarasi kesha patikana na atatangazwa kwenye uongozi wa kijiji tayari kwa kuanza kazi ndani ya mwezi huu na kwa upande wa mto Bubu tayari pesa imepatikana na kandarasi itatangazwa hili punde ili hatua za awali za kufanya upembuzi yakinifu zianze.Baada ya maswali mengi ambayo yalikua niya kujenga na yenye tija kwa Halmashauri yalijibiwa kiufasaha nakutolea maelezo na uafafanuzi wa hali ya juu kutoka wataalam ngazi ya Mkoa na halmashauri.
Baada ya kikao hicho msafara ulianza kuelekea kijiji cha Pahi katika kata ya Pahi ambako mkutano wa hadhara uliandaliwa kwa ajili ya kuongea na wananchi nakusikiliza kero zao . Msafara uliwasili saa kumi jioni nakupokelewa kwa nderemo na vifijo na wananchi wa kijiji cha Pahi na vitongoji vyake na kuanza mkutanao kwa kusikiliza kero za wananchi ambapo kero moja moja ilijibiwa na timu ya wataalam aliyo ambatana nayo. Lakini pia Mkuu wa mkoa alipata taarifa ya utekelzaji miradi katika kata ya Pahi ambapo kata inatekeleza miradi ifuatayo ,ujenzi wa kituo cha afya ambacho ujenzi wake uko katika hatua ya upauaji na kimegarimu shilingi milioni 500,Mradi wa maji wenye thamani ya milioni 34, Mradi wa ukamilishaji Zahanati katika kijiji cha Potea wenye thamani ya shilingi milioni 50 na Madarasa mawili na matundu sita ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 46 katika kijiji cha Salare.
Baada ya hapo Mheshimiwa Mkuu wa wilaya Dr,Hamisi Mkanachi alimkaribisha mgeni rasmi tayari kwa kuongea na wananchi ,Mh. Senyamule aliwahutubia wananchi wa Pahi kwa kuambia lengo la ziara yake ina mambo makuu matatu, mambo hayo ni kujitambulisha na kuangalia maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Serikali ngazi ya Halmashauri jambo la pili ni kufanya mikutano na kusikiliza kero za wananchi , watumishi na madiwani na jambo la tatu ni kutolea ufafanuzi kero ambazo zimetolewa na wananchi. Migogoro ya ardhi ni miongoni mwa maswali ambayo yalitawala sana lakini jambo hili lilitolewa ufafanuzi na afisa ardhi mkoa lakini pia aliahidi kuja na timu ya ardhi mkoa kwa ajili yakukaa pamoja na kupata ufumbuzi lakini alishauri kabla ya kuja timu ya mkoa viongozi wa vijiji na kata pamoja na wananchi wakae pamoja na kumaliza migogoro hii kwani migogoro hii huanzishwa na wananchi wenyewe kwa maslahi yao binafsi.
Jambo ambalo alitilia mkazo Mh, Senyamule ni suala la elimu katika mkoa lakini pia katika wilaya kuwa katika hali mbaya sana jambo ambalo linatoa taswira mbaya na kuonesha kua dhamira ya elimu katika wilaya iko chini na hapa alitoa maagizo kua kuanzia sasa kuwe na vikao vya wadau elimu kuanzia ngazi ya kijiji na kata vifanyike kupata tathmini ya ufaulu na kutengeneza mikakati pia mazingira ili kupandisha ufaulu na kufaham tatizo liko wapi nakutoa mda wa mwezi mmoja ili kupata mrejesho kutoka katani ikihusisha mambo matatu,
Moja mikakati ya ufaulu katika ngazi ya kata,mbili Taarifa za utoro kutoka katani na namna ambavyo wamejipanga kudhibiti jambo hili na tatu n imiundo mbinu kwenye kata hapa alilenga upungufu wa madarasa na jinsi walivojipanga kupunguza upungufu wa madarasa ikiwemo kuhamasisha wananchi kushiriki katika nguvu kazi ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuunga mkono juhudi za serikali.Mkuu wa Mkoa alisisitiza Uwajibikaji na dhana ya utawala bora hasa kwa watendaji wa vijiji kuitisha mikutano maalum na kusoma mapato na matumizi ili kuweka uwazi kwa jamii wanayo isimamia na kutekeleza miradi yote kwa wakati na kufanya ushirikishwaji kwa wananchi katika ujenzi wa miradi na hii itawafanya wananchi waione miradi ni yao waisimamie vyema na wafaham vitu ambavyo serikali inafanya kwa ajili yao na vizazi vijavyo. Mkutano ulihairishwa rasmi saa kumi na mbili jioni nakuahidi kurudi tena pahi kwa mara nyingine kwani watu wa Pahi ni Wakarimu sana.
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.