• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

BARAZA LA MADIWANI KONDOA DC LAJADILI AGENDA 8, MIRADI NA USTAWI WA WANANCHI

Posted on: February 3rd, 2026

Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo, kikilenga kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa wananchi.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, Wawakilishi wa Vyama vya Siasa , Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Akiongoza kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Mhe. Salum Mabote, amesimamia utekelezaji wa agenda zote nane (8) za kikao na kuongoza mijadala yenye tija kwa maendeleo ya Wilaya.

Katika kikao hicho, Mhe. Mabote pia amepokea na kujadili taarifa za utendaji kazi wa Kamati nne (4) za kudumu za Halmashauri, ambapo taarifa hizo zimefungua mijadala chanya iliyolenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Ndg. Shaban Millao, alipata fursa ya kujibu maswali ya papo kwa papo yaliyoulizwa na Waheshimiwa Madiwani. Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni mgogoro wa kijiji cha Kimotoro, utolewaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa makundi yenye sifa, fidia kwa Wananchi waliovamiwa na tembo na kuharibiwa mazao, pamoja na mikakati ya Wilaya katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, Ndg. Millao alisisitiza umuhimu wa Wananchi kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote, Matumizi ya Daftari la Wakazi, Upatikanaji wa lishe mashuleni pamoja na uandikishaji wa Watoto wenye umri wa kwenda shule. Vilevile aliwaasa Waheshimiwa Madiwani kuwa chachu ya utekelezaji wa agenda hizo katika maeneo yao.

Katika kikao hicho, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ndg. Erick..., aliwasilisha salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Rosemary Senyamule, na kupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa utendaji kazi mzuri na utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa amenituma kuwafahamisha kuwa anaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo na amesisitiza ikamilike kwa wakati ili ianze kuwanufaisha wananchi,” - Ndg. Erick.

Akihairisha Baraza hilo, Mwenyekiti Mabote amepongeza juhudi zilizofanyika katika Sekta ya Elimu kwa ufaulu kuongezeka kwa asilimia 95.89% katika matokeo ya Kidato cha Nne Mwaka 2025 kutoka 93.41% Mwaka 2024. Aidha amewataka Waheshimiwa Madiwani kusimamia vyema na kuyatekeleza yale yote yaliyojadiliwa katika Baraza hilo ili kuendelea kuleta tabasamu kwa Wananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA UKODISHAJI MAGARI October 16, 2025
  • MATOKEO KIDATO CHA SITA July 07, 2025
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI KONDOA DC LAJADILI AGENDA 8, MIRADI NA USTAWI WA WANANCHI

    February 03, 2026
  • DKT.ASHATU AIFUNGUA ZAHANATI YA BERABERA,KONDOA DC

    February 01, 2026
  • WAZIRI DKT.ASHATU KIJAJI ASIFU UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI KONDOA DC.

    February 01, 2026
  • INADES-FORMATION & KONDOA DC KUFIKIA MALENGO UPANDAJI MITI

    January 30, 2026
  • Fungua zaidi

Video

Umeme kufika Kituo cha Afya Mauno-Kondoa:-Mkuu wa Mkoa Dodoma
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.