• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WAZIRI DKT.ASHATU AWAFARIJI WANANCHI WA HANANG'

Posted on: December 15th, 2023

Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.Dkt Ashatu Kijaji (Mb) amejumuika pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao &Mke wake Mama Millao, Mwenyekiti wa CCM-Kondoa Bi.Hijja Suru &Ujumbe wake pamoja na Wafanyabiashara wa Kariakoo na Kondoa kuwapa faraja Wananchi wa Wilaya ya Hanang baada ya Maafa ya Maporomoko ya Tope,Mawe, Magogo pamoja na Maji kutoka Mlima Hanang Mkoani Manyara alfajiri ya tarehe 3/12/2023.

Akiongoza msafara huo Mh. Dkt.Ashatu amepokelewa na Naibu Waziri wa Ujenzi Mha.Godfrey Kasekenya kwa kumwelezea hali ilivyo kwa sasa akimpitisha maeneo yote yaliyoathirika yakisababisha Vifo,Majeruhi na Uharibifu wa Mali pamoja na kumkutanisha na baadhi ya Wananchi wakiwemo Wafanyabiashara waliokumbwa na kadhia hiyo.

Mh.Dkt Ashatu ametumia nafasi hiyo kuwafariji Viongozi wa Chama,Mbunge wa Jimbo la Hanang,Serikali pamoja na Wananchi kwa nyakati tofauti akiwaasa kumshukuru mwenyezi Mungu na Kumuomba kuwarehemu Ndg.waliofariki kwenye maafa hayo na waliobaki kuwapa nguvu kwa kuwaombea Subra.

Mh.Dkt.Ashatu amesema Uongozi wa Wafanyabiashara Kariakoo na Kondoa, Uongozi wa CCM-Kondoa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kondoa Ndg.Shaban Millao &Mkewe Mama Millao wamejumuika pamoja kuwapa Pole,Faraja na kukabidhi kidogo walichojaaliwa kupitia michango kama Utoaji Bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Tsh.Mil 68,Lak 6 na Elfu 50(Wafanyabiashara Kariakoo),Vifaa vya Shule vyenye thamani ya Tsh Mil 1(Jumuiya ya Wamachinga),Bidhaa mbalimbali kutoka kwa wadau wa Maendeleo Kondoa zikiratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kondoa pamoja na Bidhaa zenye thamani ya Tsh Mil 1(Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kondoa Ndg.Shaban Millao &Mkewe).

Mh.Dkt.Ashatu amesema Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia inaendelea kufanya tathmini na kuona nini cha kufanya yakiwemo Uratibu wa Mazungumzo Baina ya Wizara ya Fedha na Taasisi za Fedha ili kuwaongezea muda wananchi waliochukua Mikopo ili waweze kujipanga katika kipindi hiki kigumu.

Kwa niaba ya Uongozi wa Wafanyabiashara wa Kariakoo Mwe.Kamati ya Maafa Ndg.Frank Nduta amesema wameguswa na maafa hayo na kutoa wito kwa Watanzania kutoa chochote walichojaaliwa kwa ajili ya kuwafariji Wahanga wa Maafa hayo.

Pia kwa Niaba ya Uongozi wa Wilaya ya Hanang shukrani zimetolewa kwa Dkt.Ashatu na Ujumbe alioambatana nao na kuahidi kupokea misaada kwa uaminifu,kuilinda na kuifikisha kwa walengwa.

Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka Serikalini kupitia Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg.Mobhare Matinyi tarehe 13/12/2023 kwa waandishi wa habari amesema Jumla ya Miili 89 ilipatikana tangu maafa yatokee tarehe 3/12/2023,Majeruhi 139 walifikishwa Hospitali na kupatiwa matibabu kwa gharama za Serikali kupitia Agizo la Rais Dkt.Samia Suluhu ,Misaada ya Fedha,Chakula, Vitu na Vifaa kutoka kwa wahisani mbalimbali hadi kufikia tarehe 12/12/2023 kiasi cha Tsh.149,757,500 kilikusanywa kwenye Akaunti ya Mfuko wa Taifa wa Misaada ya Maafa (National Relief Fund iliyopo Benki kuu ya Tanzania(BoT).kupitia Akaunti na.National Relief Fund Na.9921159801 na Swift code TANZTZTX kwa wanaotuma Fedha kutoka Nje ya Nchi.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.