• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

Posted on: May 4th, 2025

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wakiongozwa na Mkuu wa Divisheni ya Utawala na rasilimali watu wamempongeza Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa 35.1%.

Hayo yamejiri mapema Mei Mosi ikiwa ni baada ya tamko la Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akihutubia makundi mbalimbali ya Watumishi wa Umma na Sekta binafsi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika  Viwanja vya Bombadia Manispaa ya Singida.

"Tunampongeza Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi, kwa kuwapandisha madaraja na sasa kuwaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa 35.1% kutoka Tzs.370,000 hadi Tzs.500,000.kupitia nyongeza hii itachochea hari ya kufanya kazi kwa watumishi" alisema Ndg.Peter Ngomuo, Mkuu wa Divisheni ya Utawala na raslimali Watu Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

Ndg.Ngomuo ametumia nafasi hiyo pia kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Ndg.Shaban Millao kwa niaba ya watumishi, kwa kuwezesha ushiriki wa baadhi ya watumishi waliofanikiwa kupendekezwa na watumishi wenzao kama watumishi hodari kwa Mwaka 2024/2925  kwa kuzingatia kada husika. Sherehe za Maadhimisho hayo kwa mwaka huu zilifanyika Mkoani Singida ambapo Kaulimbiu ilikuwa "Uchaguzi Mkuu 2025 utuletee Viongozi wanaojali hali na maslahi ya wafanyakazi, sote tushiriki.

Nyongeza hiyo ya mshahara inatarajiwa kuanza kutumika katika mwaka wa fedha 2025/2026, kuanzia mwezi Julai kiwango cha chini cha mshahara kuongezeka kutoka TzS. 370,000 hadi 500,000 sambamba na ngazi nyingine za mshahara nazo zitapanda kwa kiwango kizuri jinsi bajeti itakavyoruhusu.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 12, 2025
  • RC SENYAMULE AFANYA ZIARA KONDOA DC

    May 13, 2025
  • ELIMU YA UZUIAJI UPOTEVU WA NAFAKA KUWA SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA KONDOA DC

    May 11, 2025
  • WANANCHI KIJIJI CHA ITUNDWI WAADHIMISHA KWA VITENDO SIKU YA AFYA NA LISHE

    May 07, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.