Tukio la ugawaji vishikwambi limefanyika leo tarehe 16January ,2023 katika viunga vya makao makuu ya Halmashauri yalioko katika kijiji cha Bukulu kata ya Soera Wilayani Kondoa.Akiongoza zoezi hilo Afisa Elimu Msingi na Awali Bi Margareth Temu akiwa na timu nzima ya Elimu msingi na Sekondari waliongoza zoezi hilo ,zoezi ambalo lilihusisha walengwa wakuu ambao ni Walimu wa shule za Msingi,Walimu wa shule za Sekondari pamoja na Maafisa Elimu kata wote kutoka kata zote 21 za Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Katika zoezi hilo Bi Temu alikua na haya ya kusema na hapa namnukuu'' Lengo kuu la Serikali kutoa vishikwambi hivi vipatavyo 896 kwa walimu wote wa Sekondari na Msingi pia kwa Maafisa Elimu kata wote ni kurahisisha tendo la ufundishaji na ujifunzaji ,tunamshukuru Mh,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuliona hili na kuwapa Walimu kifaa hiki muhimu ili kuinua kiwango na ubora wa Elimu Tanzania.
Wakipokea vitendea kazi hivi, Mwl Adam P. Faraji kwa niaba ya Walimu wote alikua na haya ya kusema'' Kwa niaba ya walimu wote natoa shukrani za dhati kwa serikali kwa kutupatia vishikwambi hivi ,ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji mashuleni kwa vitaleta chachu kwa walimu kujifunza na kupakua vitabu mbali mbali vya kiada na ziada ambavyo vitasaidia kuinua taaluma ndani nje ya Wilaya ya Kondoa''.
Lakini pia Afisa Elimu Sekondari Bi Line Chanafi aliwasisitiza walimu hawa kutunza vishikwambi hivi na kuvitumia kwa lengo lililo kusudiwa na Serikali katika kuboresha na kuinua taaluma mashuleni.Hakika limekua ni jambo la kihistoria katika tasnia ya elimu alisikia Mwalimu mmoja akisema.
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.