• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

UPASUAJI WA KIBINGWA WA KUUNGANISHA UTUMBO MDOGO WAFANYIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KONDOA.

Posted on: October 1st, 2024

Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa iliyopo Bukulu kwa mara ya kwanza imefanya Operesheni ya kwanza ya Kibingwa ya kukata kipande cha utumbo mdogo na kuunganisha utumbo huo baada ya kujikunja.

Hayo yamefanywa na Madaktari Bingwa wa Rais Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na timu ya wataalam wa afya kutoka halmashauri ikiwa ni awamu ya pili ya  utoaji huduma za kibingwa  na ubingwa bobezi kwa halmashauri za Mkoa wa Dodoma kupitia hospitali zake.

Operesheni hiyo imefanywa na Dr.Lukiza Kamhabwa (Bingwa wa upasuaji/bobezi wa mfumo wa mkojo) kwa mgonjwa aliyepewa jina la I.D.N mwenye miaka 42 mkazi wa kijiji cha Sakami Akimfanyia upasuaji wa kukata kipande cha utumbo mdogo na kuunganisha baada ya utumbo huo kujikunja kutokana na uvimbe katika utumbo mdogo.

Sambamba na Operesheni hiyo ya kibingwa pia Mwanamke aliyepewa jina la M.S.H wa miaka 27 kutoka Sakami alifanyiwa upasuaji wa kutoa uvimbe kwenye via vya uzazi na Dr Emiliana Mvungi

(Bingwa wa magonjwa ya wanawake na ukunga) uliomtesa kwa miaka 10 na Mwanaume mwenye jina H.I.M mwenye umri wa miaka 96 aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la ngiri (Hernia)iliyomsumbua kwa miaka 5 alifanyiwa upasuaji kwa njia ya kisasa (Hernioplasty).

Katika huduma hizo za kibingwa wagonjwa walionufaika na ujio wa madaktari bingwa ni 381kupitia mchanganuo wa Magonjwa ya ndani walikua 119, magonjwa yanayohitaji upasuaji 67, magonjwa ya Watoto 85 na magonjwa ya akinamama 111.

Kwa upande viongozi wa Halmashauri   wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Shaban Millao na Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Elimu na Maji  Mhe.Rahim  Salum walipata wasaa wa kuzungumza na wananchi waliojitokeza kupata matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi na kuzungumza na jopo la madaktari hao wa kibingwa.

Ndg.Millao alitumia fursa hiyo kumshukuru Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

kwa jitihada zake za kuhakikisha wananchi wengi wanafaidika na huduma hizo za kibingwa, jitihada za Mhe.Dkt Ashatu Kijaji (Mb) kwa kuwapambania wananchi wa Jimbo la Kondoa dhidi ya huduma za afya, Watumishi wa Vituoni, Mwenyekiti wa huduma za jamii pamoja na timu ya uendeshaji wa huduma za afya kwa kusimamia zoezi zima.

Pamoja na kuwahudumia wananchi waliojitokeza katika hospitali hiyo kwa upande wa watoa huduma za afya wa Halmashauri walipata mafunzo elekezi kazini (Mentorship)kutoka kwa madaktari bingwa wa Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Huduma za kibingwa na bobezi kwa awamu ya pili  zimetolewa katika Halmashauri ya wilaya ya Kondoa kuanzia tarehe 24 hadi 28 Septemba, 2024 kwa wananchi (wagonjwa waliojitokeza) wakipatiwa huduma za kibingwa kwa magonjwa ya wanawake na ukunga, watotona watoto wachanga, magonjwa ya ndani na upasuaji katika mfumo wa mkojo kama sehemu ya jitihada za Mhe.Rais Dkt.Samia katika kuhakikisha wananchi wengi wanafaidika na huduma hizo za kibingwa na bobezi.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 12, 2025
  • RC SENYAMULE AFANYA ZIARA KONDOA DC

    May 13, 2025
  • ELIMU YA UZUIAJI UPOTEVU WA NAFAKA KUWA SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA KONDOA DC

    May 11, 2025
  • WANANCHI KIJIJI CHA ITUNDWI WAADHIMISHA KWA VITENDO SIKU YA AFYA NA LISHE

    May 07, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.