• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

UGAWAJI PIKIPIKI KUONGEZA UFANISI KWENYE KILIMO NA MIFUGO KONDOA DC

Posted on: December 16th, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imekabidhi vyombo vya moto aina ya pikipiki   6 zenye thamani ya Tsh 17,400,000 kwa Awamu ya pili kwa Maafisa ugani kwa lengo la  kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi.

Akikabidhi vitendea kazi hivyo Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mh.Dkt Ashatu Kijaji amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia SuluhuvHassan kwa kuwafikia Wakulima na Wafugaji na kuendelea kuwawezesha Maafisa ugani kupata vitenda kazi ngazi ya Kata zote 21 za halmashauri  kwa kuwa na jumla ya pikipiki 22 baada ya nyongeza ya pikipiki 6 kutoka 16 za awamu ya kwanza.

Mh. Dkt Ashatu amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imeshikilia Uchumi wa Taifa kwa kuilisha Dodoma kupitia shughuli za Kilimo na Ufugaji akiwaasa maafisa ugani kuwasaidia Mawaziri wa Kisekta kwa kuwaongezea ufanisi Wakulima na Wafugaji baaada ya kupata vitendea kazi ikiwemo kipimia udongo, vyombo vya usafiri ili Kukuza uchumi wa Tanzania katika soko la kimataifa kupitia Bidhaa mbalimbali kama Nyama bora na Mazao pamoja na kuhakikisha wanavitunza vyombo hivyo.

Bi. Hijja Suru ambaye ni  Mwenyekiti CCM - Kondoa amesema vitendea kazi hivyo vikarahisishe shughuli za utoaji Elimu ya kutosha kwa Wakulima kupitia matumizi sahihi ya Mbegu kwa kuleta mabadiliko kwa Wakulima.

Kwa upande wake katibu Tawala Wilaya ya Kondoa Bi. Christina Kalekezi amesema kilimo ni uti wa mgongo kiu ya Viongozi ni kuona Taifa linapata chakula cha kutosha na ufugaji wenye tija kwa kufuata kanuni za ufugaji na kuhimiza upatikanaji wa mafuta yatakayosaidia kufikiwa Wakulima kwa wakati ili kuondoa visingizio visivyokua na ulazima.

Kwa niaba ya Maafisa Ugani, Ndg. Plasid Masumbuko, ambaye ni Afisa Ugani mnufaika toka Kata ya Kalamba, ametoa shukrani kwa Rais kwa mwendelezo anaouonesha wa kuwezesha sekta ya kilimo na mifugo na kuahidi kuvitumia vyombo hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kukuza uchumi wa wakulima kwa kilimo chenye tija baada ya kupata vitendea kazi.

Awali akiwasilisha taarifa yake kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ndg.Juvenal Munishi amesema kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Rais Dkt Samia Suluhu imetoa fedha za Ununuzi wa pikipiki 6 Awamu ya pili zenye thamani ya Tsh 17,400,000, Awamu ya kwanza halmashauri ilipokea pikipiki 16 zenye thamani ya Tsh 38,400,000 za Maafisa ugani kupitia wizara ya kilimo na kufikisha jumla ya pikipiki 22.

Akihitimisha halfa hiyo ya kukabidhi pikipiki Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao amesema vyombo hivyo vitaimarisha sekta ya kilimo na mifugo akihakikisha Bajeti ya upatikanaji wa mafuta inatengwa na kuwataka wanufaika wa vyombo hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao ili kusaidia upatikanaji wa Mapato.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.