• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Ubalozi wa Japan Kujenga Sekondari Keikei Kondoa DC

Posted on: March 6th, 2019

Ubalozi wa Japan umeahidi kujenga Shule ya Sekondari ya kata ya Keikei ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya kata ya Busi inayohudumia wanafunzi wa kata mbili.

Ahadi hiyo ilitolewa na mwakilishi wa ubalozi wa Japan Bwana Takao Kurukawa katika kata ya Keikei alipofika katika eneo lililotengwa  kwaajili ya ujenzi wa sekondari hiyo hivi karibuni.

“Nimekuja kuangalia eneo ambalo litajengwa Shule ya  Sekondari na ubalozi wa Japan baada ya kupokea maombi ya kuomba kujengewa shule kutoka Halmashauri ya Wilaya  ya Kondoa “Alisema Bwana Takao

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezeria Makota aliwashukuru ubalozi wa Japan kwa msaada wao na kuwataka wananchi wa Keikei kujitoa kwa hali na mali ila kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kuwahudumia wananchi.

“Shukrani za dhati ziende kwa Mbunge Mhe.Ashatu Kijaji kutokana na agenda yake ya kuhamasisha elimu na sasa anatekeleza kwa vitendo baada ya kuona watoto wengi wanafaulu na kwenda shule ya Sekondari Busi hali iliyopelekea kuwa na upungufu wa madarasa hivyo mheshimiwa mbunge akaamua kwenda kuomba msaada ubalozi wa Japan na leo wamekuja.” Alisema Mhe.Makota

Hata hivyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Kondoa Mustapha  Semwaiko alisema kuwa katika Kata 21 za Halmashauri ya Wilaya  ya Kondoa ni Kata ya Keikei pekee ambayo haikuwa na Sekondari ya Kata na kulikuwa na ufaulu mkubwa wa wanafunzi ambao ulisababisha msongamano katika Sekondari ya Busi na kupelekea kuwe na upungufu wa madarasa.

“Kutokana na kuwa na tatizo la madarasa Shule ya Sekondari ya Busi tulishirikiana na  Mheshimiwa Mbunge tukapiga hodi katika ubalozi wa Japan ambao walikubali na watatujengea madarasa 8, matundu ya vyoo 10 na ofisi 2 za walimu na sisi tumetenga eneo la ekeri18 kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo.”Alisisitiza Mustapha

Mmoja wa wananchi wa Kata hiyo Bwana Juma Ramadhani aliwashukuru viongozi wote walioshiriki katika kufanikisha jambo hilo kwa kuwa watoto wao walikua wakitembea umbali mrefu kufuata Sekondari katika kata jirani.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.