• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

STAKABADHI GHALANI MUAROBAINI ENDELEVU KWA WAKULIMA WILAYA YA KONDOA

Posted on: June 25th, 2025

Wafanyabiashara Kondoa wametakiwa kutumia Mfumo wa Stakabadhi ghalani unaotumika katika mauzo ya Mazao ya Ufuta, Dengu na Mbaazi ili kupata Bei Nzuri na endelevu.

Hayo yamebainishwa katika Kikao cha Baraza la Biashara Wilaya ya Kondoa kilichofanyika tarehe 23/06/2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kondoa.

Kikao hicho kilichongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Wilaya ya Kondoa Ndg. Ally Mbena, likijadili pamoja na mambo mengine namna bora ya kuuza mazao kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ambapo ilikubaliwa kwa pamoja kuwa elimu na hamasa kuhusu mfumo huu iendelee kutolewa, kutokuuza mazao husika nje ya mfumo na  kuhakikisha ushiriki kamilifu wa wafanya biashara wa mazao ambao ni sehemu muhimu ya kukusanya na kuuza mazao husika katika Vituo vilivyoainishwa kwa  Halmashauri zote mbili, za Kondoa Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

Hadi Sasa, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imeshauza Tani 822.4 za zao la Ufuta Vituo 2 vya Minada vya Kwadelo tani  209 na Kituo cha Chubi kilichopo Kata ya Itaswi zimeuzwa tani 613.4.

Jumla ya Vyama vya Msingi vya Mazao (AMCOs) vipatavyo Vinne vya Nguvumoja AMCOs LTD cha ITASWI, PUBUI AMCOs LTD kinachohudumia Kata za Pahi na Bumbuta, Kwadelo AMCOs LTD( Kata ya Kwadelo) na UMOJA AMCOs LTD kilichopo Kata ya Keikei.

Awamu ya pili ya utoaji wa Elimu na Uhamasishaji utaendelea tena kuanzia mwanzoni mwa Mwezi Julai 2025, ambao utakuwa mahsusi kwa zao la Mbaazi kuendelea kuuzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.

Kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa zinazalisha kwa wingi zao la Mbaazi, ambapo takribani Tani 15,500 zinatarajiwa kuuzwa Kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa Msimu huu wa 2024/2025.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • ELIMU YA BAJETI YA MLENGO WA KIJINSIA KUINUFAISHA KONDOA

    June 26, 2025
  • STAKABADHI GHALANI MUAROBAINI ENDELEVU KWA WAKULIMA WILAYA YA KONDOA

    June 25, 2025
  • WALIMU NA MAAFISA ELIMU KATA KONDOA DC WAJENGEWA UWEZO WA USIMAMIZI UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI

    June 21, 2025
  • WARAGHIBISHI MASUALA YA KIJINSIA WILAYA YA KONDOA WAJENGEWA UWEZO

    June 21, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.