• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

SEKONDARI YA NTOMOKO YAANZA KUPOKEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2024

Posted on: January 9th, 2024

 SEKONDARI MPYA NTOMOKO YAANZA KUPOKEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2024

Shule Mpya ya Sekondari Ntomoko iliyopo kijiji cha Ntomoko kata ya Haubi imeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mara ya kwanza baada ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo mpya na kufunguliwa kama shule nyingine nchini kuanza masomo tarehe 08/01/2024.

Akizungumza na wanafunzi hao wa kidato cha kwanza Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bi.Line Chanafi ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha shuleni hapo akiwaasa wazazi na wanafunzi ,kutumia fursa hii adhimu kuwatia moyo wanafunzi ambao bado hawajaripoti shuleni kuanza kufika.

‘’Serikali ya Mama Samia imewekeza fedha nyingi kwa kujenga miundombinu rafiki na matarajio yetu nikuwa na wanafunzi 72, niwahamasishe na kuwatia moyo wanafunziwenzenu waliopo nyumbani waweze kufika shuleni hata kama hawana sare za shule tutawapokea,tunakwenda kuwa miongoni mwa shule bora na utaratibu wa chakula utaanza mapema ‘’.alisema Bi.Chanafi.

Akiwa shuleni hapo amekabidhi na kupanda miche ya matunda,kivuli pamoja na maua akishirikiana nao kwa ajili ya kuendelea kupendezesha mandhari ya shule na kukabidhi vifaa vya kufanyia usafi.

Kwa upande wa baadhi ya wanafunzi hao wa kidato cha kwanza wamemshukuru mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea shule hiyo mpya ambayo itawapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu hadi kufikia shule ya Sekondari Intella na kuahidikufanya vizuri masomo yao.

Pia katika ziara yake ,Afisa Elimu Sekondari Bi.Chanafi ametembelea shule nyingine za sekondari Aman Abeid Karume na Kiteo zilizopo kata ya Pahi kujionea mahudhurio ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na vidato vingine,kufanya mazungumzo na walimu wa shule hizo pamoja na kutembelea mashamba ya shule kwa ajili ya uzalishajii wa mazao ya chakula kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za chakula mashuleni akiambatana na Afisa kilimo na mifugoi na uvuvi wa halmashauri Ndg.juvenal Munishi pamoja na afisa elimu sekondari taaluma Ndg.boniface chipana.

Shule Mpya ya Sekondari Ntomoko imegharimu kiasi cha Sh.MiL 544,225,626 hadi Ujenzi kukamilika Na kupata Usajili wa nambari S.422 mapema mwaka 2023.

Habari na chanzo chetu www.kondoadc.go.tz.

 

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.