• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI AKAGUA UTEKELEZAJI WA KAMPENI YA CHANJO NA UTAMBUZI WA MIFUGO KONDOA DC

Posted on: July 22nd, 2025

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini Dkt.Edwin Mhede amekagua utekelezaji wa Kampeni ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo uliofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

Haya yamejiri mapema Julai 21, 2025 akiambatana na mwenyeji wake Afisa Tarafa ya Pahi Bi.Mwasiti Kaweji kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kondoa na timu ya wataalam kutoka halmashauri na wizarani wakishuhudia utekelezaji wa kampeni hiyo kwa mifugo jamii ya Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo na Kuku katika kijiji cha Soera.

"Serikali imeweka kipaumbele kwenye sekta ya Mifugo ikilenga kukuza uchumi wa wananchi wake,ikileta 50% ya ruzuku ya chanjo na 100% ya ruzuku ya uendeshaji wa zoezi hili la uchanjaji. Uchanjaji huu ni kwa ajili ya kulinda Afya ya mifugo kwa kumpatia kinga itakayomfanya asiambukizwe homa ya mapafu (Ng'ombe), Sotoka (Mbuzi na Kondoo)na Tatu moja (Kuku)."alisema Dkt.Mhede.

Dkt.Mhede katika zoezi hilo amekabidhi vyombo vya usafiri (pikipiki 23) pamoja na vifaa mbalimbali vitakavyotumika katiza zoezi la uchanjaji na utambuzi wa mifugo kwa maafisa ugani wa mifugo halmashauri akiwataka kwenda na falsafa ya kazi iendelee.

Kwa upande wake Bi.Mwasiti Kaweji kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, amemshukuru Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha Uzinduzi wa kampeni ya chanjo na utambuzi wa mifugo nchini, halmashauri ya wilaya ya kondoa ikinufaika na vifaa mbalimbali vya chanjo, vitendea kazi kwa maafisa ugani (pikipiki23) ukilenga kukuza uchumi wa wananchi wa kondoa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao ameahidi usimamizi wa halmashauri katika utekelezaji wa uchanjaji wa mifugo iliyopo ili zoezi lifanyike kwa ufanisi mkubwa, akipongeza juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha mazingira ya ufanisi kwa maafisa ugani ambayo yatachagiza ukuaji wa sekta ya Mifugo na Uvuvi.

Nao baadhi ya Wananchi wemeipongeza Serikali kupitia Wizara yake ya Mifugo na Uvuvi, ikiwakumbuka wafugaji dhidi ya usalama wa afya za mifugo yao wakiahidi kutoa ushirikiano kwa maafisa ugani wa mifugo waliopo kwenye vijiji vyao.

Kampeni hii ilizinduliwa rasmi na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  mkoani Simiyu mapema Juni 16, 2025 ambayo halmashauri ya wilaya ya kondoa ni halmashauri nufaika nchini ikipokea vifaa na chanjo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikilenga kudhibiti magonjwa ya kipaumbele kwa mifugo ikiwa ni pamoja na Homa ya Mapafu ya N'gombe (CBPP-Dozi 200,000), Sotoka ya Mbuzi/Kondoo (PPR-Dozi 280,000) na Mdondo kwa kuku(Tatu Moja-Dozi 460,000) utekelezaji wake ni wa miaka mitano.

Chanjo hizi zitatolewa kwa gharama nafuu ambapo Chanjo ya Homa ya Mapafu ya N'gombe (CBPP)na Sotoka ya Mbuzi/Kondoo itagharimu Tzs 500 tu kwa mfugo mmoja pamoja na Chanjo za Mdondo kwa Kuku (NCD-Tatu moja) bila malipo.

Kulingana na Sensa ya Mifugo ya mwaka 2019/2020 Halmashauri ina jumla ya mifugo ipatayo 1,272,533 ikitarajia kuchanja zaidi ya Ng'ombe 351,000 Mbuzi 295,000 Kondoo Elfu 78 Kuku 542,000 pamoja na zaidi ya Nguruwe zaidi ya Elfu 4.

Matangazo

  • MATOKEO KIDATO CHA SITA July 07, 2025
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI AKAGUA UTEKELEZAJI WA KAMPENI YA CHANJO NA UTAMBUZI WA MIFUGO KONDOA DC

    July 22, 2025
  • WATUMISHI KONDOA DC WANOLEWA MFUMO WA E-UTENDAJI

    July 12, 2025
  • KONDOA DC YAJIPAMBANUA UFAULU MATOKEO YA MOCK MKOA 2025

    July 12, 2025
  • WATAALAM WA ELIMU KONDOA DC WAPIGWA MSASA KWA VITENDO ELIMU YA UOTESHAJI MICHE YA MITI

    July 12, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.