• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKUU WA MKOA WA DODOMA AKAGUA MIRADI KONDOA DC

Posted on: October 23rd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika ziara hiyo, Mhe. Senyamule alitembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa iliyopo eneo la Bukulu, ambapo alikagua ujenzi na ukamilishwaji wa majengo mapya ya hospitali pamoja na kuangalia hali ya ustawi wa jamii katika eneo hilo.

Akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Mhe. Fatma Nyangasa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Ndg. Shaban Millao, na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kondoa, Bi. Christina Kalekezi, Mhe.Rosemary Senyamule  alitembelea pia mtoto Bisadya Idd Bakari (11), anayepatiwa matibabu katika Hospitali hiyo baada ya kuungua kwa moto.

Aidha, Mkurugenzi Millao alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuipatia Halmashauri hiyo fedha zaidi ya shilingi bilioni 4.3 kwa ajili ya ujenzi wa zaidi ya majengo 14 ya hospitali hiyo, ambayo baadhi yake yameanza kutoa huduma bora kwa wananchi.

 “Tumeendelea kupokea fedha za kuendeleza miradi hii. Mwezi uliopita tumepokea shilingi milioni 800 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya dharura. Tutahakikisha tunakamilisha kazi hizi kwa ubora unaotakiwa na kwa kasi inayolingana na maelekezo ya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa,” alisema Mkurugenzi Millao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Kondoa kwa ushirikiano wao na kwa kujali ustawi wa wananchi, hasa kusimamia maendeleo na matibabu ya mtoto Bisadya, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha huduma za kijamii na afya katika maeneo yote ya mkoa.

“Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya afya kupitia ununuzi wa dawa, vifaa tiba, na kuongeza wataalamu ili wananchi wapate huduma bora katika vituo vya afya. Tunahimiza jamii kuachana na tiba potofu zisizo na uthibitisho wa kitaalamu,” alisisitiza Mhe. Senyamule.

Akihitimisha ziara yake, Mhe. Senyamule amewataka watumishi wa umma na wananchi wote wa Wilaya ya Kondoa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.

Matangazo

  • TANGAZO LA UKODISHAJI MAGARI October 16, 2025
  • MATOKEO KIDATO CHA SITA July 07, 2025
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • DC NYANGASA AKABIDHI VYOMBO VYA USAFIRI KWA WATENDAJI KATA

    October 24, 2025
  • KONDOA DC YATOA ZAIDI YA MILIONI 758 ZA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

    October 24, 2025
  • MKUU WA MKOA WA DODOMA AKAGUA MIRADI KONDOA DC

    October 23, 2025
  • DC NYANGASA ATAKA KASI KUONGEZEKA MIRADI YA KONDOA DC

    September 17, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.