• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KONDOA AFANYA ZIARA KIJIJI CHA KWAYONDU

Posted on: May 11th, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao amefanya ziara siku ya tarehe 6/05/2025 na kutembelea katika kijiji cha Kwayondu kuzungumza na wanachi.

Katika ziara hiyo Ndg. Millao amekutana na wananchi wa kijiji cha Kwayondu kusikiliza kero pamoja na kufuatilia maendeleo ya kijiji hicho , ziara hiyo iliambatana na zoezi la upandaji wa miti katika zahanati ya kijiji hicho ikiwa ni juhudi za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha na kutunza mazingira.

Akizungumza na wananchi Ndg. Millao amewaomba wananchi kuachana na matumizi ya kuni badala yake watumie majiko banifu ambayo ni rafiki kwa mazingira.

 "Nimefurahi mazingira yenu ni mazuri lakini niendelee kuwasisita tutunze mazingira, pale inapobidi tuache kutumia kuni badala yake tutumie majiko ya banifu". Alisema Ndg.Millao

Aidha Ndg.Millao amewaasa wananchi kujitokeza kushiriki zoezi la uchaguzi mkuu wa serikali kwa kuwapigia kura viongozi ambao ni wazalendo, wapenda haki na wenye nia ya dhati ya kufanya maendeleo katika taifa letu "Tujitokeze kwa wingi kuchagua viongozi wenye maono, Viongozi wanao sisitiza amani na utulivu, kiongozi mwenye uchungu na kina mama ,wakulima pamoja na sekta zote za maendeleo ya jamii" alisema Ndg. Millao.

Wananchi wa kijiji cha Kwayondu wameishukuru serikali kwa jitihada ambazo inafanya katika kuhakikisha maendeleo yanafika mpaka ngazi ya vijiji, sambamba na hilo wananchi wamemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg. Shaban Millao kwa kuahidi kumalizia zahanati yao waliyoanzisha kwa nguvu za wananchi pamoja na kusikiliza changamoto zao ambazo ameahidi kufikisha salamu hizo kwa serikali ili ziweze kufanyiwa kazi mara moja.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • VIONGOZI WA ELIMU NA WAKUU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KONDOA DC WANOLEWA KUHUSU MFUMO WA UTHIBITI UBORA WA SHULE KIDIGITALI

    May 14, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA SOERA

    May 13, 2025
  • DED MILLAO AHIMIZA USIMAMIZI MPANGO WA UTUNZAJI MAZINGIRA KONDOA DC

    May 12, 2025
  • MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KONDOA AFANYA ZIARA KIJIJI CHA KWAYONDU

    May 11, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.