• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

Posted on: April 16th, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao amewaongoza wananchi wa kata ya Mnenia katika Bonanza la Michezo katika kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2025.
Akizungumza katika Ufunguzi wa Bonanza hilo Ndg.Millao , amesema lengo kuu la kuanzisha Bonanza hilo ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwa kushiriki kikamilifu katika mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru ambao utapokelewa katika kata ya Mnenia tarehe 23 Aprili ,2025.
"Kujitokeza kwetu kwa wingi inadhihirisha kuwa tuna imani na Serikali yetu inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,hivyo jukumu letu ni kuhakikisha tunahamasishana kwa idadi kubwa na kujitokeza siku hiyo."alisema Ndg.Millao.
Sambamba na hilo Ndg.Millao amewahamasisha wananchi kuchagua viongozi wenye uchungu na maendeleo ambao watakua na nia ya kudumisha Amani na Upendo,akiwasisitiza kulinda amani iliyoasisiwa na muasisi wa taifa letu Mwl.Julius K.Nyerere na kujifunza kwa nchi jirani zinavyoteseka baada ya kukosa amani.
Kwa upande wake Afisa Utamaduni Halmashauri Ndg.Mohamed Chillo amewashukuru viongozi wa kata hiyo kwa kuandaa Bonanza hilo,akiwaasa wananchi kuwa tayari katika ushiriki wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2025.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnenia Mhe.Abdi Ally Chobu ameushukuru uongozi wa Halmashauri kwa kuchagua Kijiji cha Mnenia,kuwa kituo cha Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2025.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 unatarajiwa kupokelewa tarehe 23 Aprili 2025, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kijiji cha Mnenia na kukesha katika kijiji cha Kisese Disa-Kata ya Kisese ikiongozwa na kauli mbiu isemayo "Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu "
Mwenge wa Uhuru utatembelea ,kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo : Uzinduzi wa Mradi wa Mazingira na Usafi katika Zahanati ya Itundwi, Ujenzi wa Madarasa, Ofisi na Matundu ya vyoo Shule ya msingi Bambare, Ujenzi wa Daraja la Mto Hurui- kijiji cha Hurui, Mwenge wa Uhuru pia utakagua miradi miwili ambayo ni Mradi wa Nishati safi kijiji cha Mnenia, Mradi wa Kikundi cha Vijana Electronic kijiji cha Kisese Dissa, Mwenge wa uhuru pia utapita katika miradi miwili kuweka mawe ya msingi katika Mradi wa maji uliopo kijiji cha Bambare na Mradi wa Ofisi ya kijiji uliopo kijiji cha Filimo.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 12, 2025
  • RC SENYAMULE AFANYA ZIARA KONDOA DC

    May 13, 2025
  • ELIMU YA UZUIAJI UPOTEVU WA NAFAKA KUWA SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA KONDOA DC

    May 11, 2025
  • WANANCHI KIJIJI CHA ITUNDWI WAADHIMISHA KWA VITENDO SIKU YA AFYA NA LISHE

    May 07, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.