• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKURUGENZI KONDOA DC AUDHURIA SHAMBA DARASA KUHAMASISHA KILIMO BORA

Posted on: May 6th, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao amehudhuria mafunzo ya kilimo "Shamba Darasa"na Wakulima akihamasisha kilimo Bora.

Hayo yamejiri mapema Mei 21kata ya Soera, kijiji cha Bukulu yakiwakutanisha wakulima wa kata hiyo na vijiji na vijiji jirani wakishiriki tukio hilo lenye lengo la kukuza na kuhamasisha kilimo bora, Shirika lisilo la kiserikali Rikolto likiwa mwandaaji wa mafunzo hayo.

Akifungua mafunzo hayo Ndg.Millao ambaye alikua  Mgeni rasmi, ameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira rafiki kwa wadau wa kilimo kupata fursa ya kutoa elimu katika sekta ya kilimo.

"Ni lazima tuishukuru Serikali kwa kuandaa mazingira mazuri ambayo yanawakaribisha wadau mbalimbali wa kilimo ambao ndio chanzo cha sisi kukutana mahali hapa leo ,Sisi ni moja kati ya Wilaya Saba zinazofaidika na mradi huu nchini"alisema Ndg.Millao.

Katika hatua nyingine Ndg.Millao amewahimiza wananchi hao kushiriki kikamilifu zoezi la Uchaguzi mkuu wa viongozi kwa nafasi ya Rais,Wabunge na Madiwani ifikapo mwezi Oktoba kwa amani na utulivu pamoja na Uboreshaji wa taarifa na kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga kura awamu ya pili katika muda uliobaki kwa wale wenye sifa.

Awali katika taarifa yake Bwana Shamba Ndg.Godfrey Mwenda kutoka Rikolto amesema shirika hilo limetoa elimu kwa zaidi ya wakulima 8000 na mafunzo mengine yaliyotolewa kwa wakulima namna ya kulinda mazao yao yakiwa shambani na baada ya kutoka shambani,akiishukuru timu ya maafisa ugani kwa kufikisha elimu hiyo kikamilifu kwa wakulima.

Naye Diwani mwenyeji wa kata hiyo Mhe.Jamilah Gamaha amelishukuru Shirika hilo kwa elimu yao nzuri inayotolewa kwa wakulima kwakua ni chachu ya mabadiliko katika upande wa kilimo,akiwaasa wakulima wayafuate yale ambayo yametolewa na wataalam.

Tukio hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka taasisi za kifedha ikiwemo Benki,Wanunuzi wa mazao,Wakulima,Wadau wa Mbegu n.k.

Shirika la Rikolto linatekeleza Mradi wa Vijana Kilimo Biashara (VKB)katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa likiwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo Alizeti,Mtama,Mbogamboga na Matunda likiwahamasisha wakulima kutumia pembejeo zilizobora ili kuongeza uzalishaji,kumwezesha mkulima kulinda upotevu wa mazao.Katika kuyafikia malengo shirika hilo limeanzisha Mashamba darasa 14 kwenye kata 8 ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 12, 2025
  • RC SENYAMULE AFANYA ZIARA KONDOA DC

    May 13, 2025
  • ELIMU YA UZUIAJI UPOTEVU WA NAFAKA KUWA SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA KONDOA DC

    May 11, 2025
  • WANANCHI KIJIJI CHA ITUNDWI WAADHIMISHA KWA VITENDO SIKU YA AFYA NA LISHE

    May 07, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.