• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MAKAMU WA RAIS MHE.DKT MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI DARAJA LA HURUI-KONDOA DC

Posted on: August 21st, 2024

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Philip Isdor Mpango ameweka jiwe la msingi katika Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Hurui ,lenye Urefu wa Mita 30 linalotekelezwa na Serikali kwa kutumia chanzo cha fedha kutoka Tozo za Mafuta (Fuel Levy)Tsh Bil 1.6 ambalo linaunganisha Mkoa wa Dodoma na Manyara.

Hayo ameyafanya akiwa katika ziara yake Mkoani Dodoma ikiwa ni siku ya Tatu baada ya kuzifikia Halmashauri 5 kati ya 8 akiambatana na jopo la Manaibu Waziri wa Kisekta wakiongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Festo Dugange.

Mhe.Mpango baada ya uwekaji Jiwe la Msingi katika Daraja hilo ameagiza Wakala wa Barabara Mijini na Vijiji(TARURA)kufanya Ukarabati wa Barabara ya Ntundwa-Hurui (Kondoa)ili kurahisisha Shughuli za Kiuchumi, Wananchi wa Kata ya Kikore na Watumiaji wa Daraja hilo kulitunza na kuotesha miti maeneo yote ya Mto Hurui  ili kuokoa Daraja hilo lisiharibike kutokana na Uharibifu wa Mazingira.

Mhe.Mpango ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa bidii yake ya kuwaletea Maendeleo Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa akitoa Zaidi ya Tsh Bil 77 miradi ya Kisekta ikiwemo Elimu, Afya ,Maji na Barabara pamoja na juhudi za Mhe.Dkt Ashatu Kijaji (Mbunge wa Jimbo la Kondoa)&Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Mazingira na Muungano akiwapambania wananchi wa jimbo lake.

Kwa upande wa Wizara za Kisekta ameziagiza ;Wizara ya Maji kukamilisha Mradi wa Maji unaotekelezwa katika Kata hiyo ifikapo tarehe 30/10/2024,Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kushirikiana na Mbunge wa Jimbo kushughulikia changamoto iliyotolewa na Wananchi  wa Hurui dhidi ya Ardhi ya kijiji kuuzwa kwa Mwekezaji bila kufuata utaratibu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutenga fedha za Ujenzi wa Bweni, Sekondari ya Kikore baada ya Ahadi yake kwa Wananchi wa kata Kikore pamoja na Wananchi wa Kata hiyo kutenga Eneo lenye Ekari 15 kwa ajili ya Kujengewa Kituo cha Afya.

Sambamba na hayo Mhe.Dkt Mpango amepokea Taarifa ya Wizara ya Nishati dhidi ya Usambazaji Umeme Ngazi ya Vitongoji Nchi ikiwemo vitongoji vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa baada ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dotto Biteko kusaini Mkataba na Mkandarasi.

Awali akimkaribisha Makamu wa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amemwomba Mhe.Dkt.Mpango kufikisha salamu na shukrani kwa Rais,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikia wananchi kupitia fedha za miradi ya Kisekta.

Naye Diwani mwenyeji wa kata ya Kikore Mhe.Ngware kwa furaha na bashasha ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ikiwafikia wananchi kwa kuwajengea Daraja hilo ikiwa ni baada ya Daraja lililokuwepo awali kuharibiwa na maji mwaka 2019 na kuahidi kulitunza.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 12, 2025
  • RC SENYAMULE AFANYA ZIARA KONDOA DC

    May 13, 2025
  • ELIMU YA UZUIAJI UPOTEVU WA NAFAKA KUWA SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA KONDOA DC

    May 11, 2025
  • WANANCHI KIJIJI CHA ITUNDWI WAADHIMISHA KWA VITENDO SIKU YA AFYA NA LISHE

    May 07, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.