Leo tarehe 14/06/2023 yamefanyika makabidhiano ya ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa katika ukumbi wa mikutano ulioko ndani ya jengo la utawala makao makuu yaliyoko katika kijiji cha Bukulu kata ya Soera.Katika makabidhiano hayo yaliyo mhusisha Mustapha S Yussuf aliekua Mkurugenzi wa Halmashauri na Ndugu Shabani K Millao ambae ni Mkurugenzi mpya kufuatia uteuzi mpya wa wakurugenzi alioufanya Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Akikabidhi Ofisi wa Mteule mpya Ndugu Semwaiko alisema nikiwa kiongozi nimefanya mengi mazuri kwa kushirikiana nanyi katika kuiletea kondoa maendeleo lakini pia kutizimiza azma ya serikali katika kusimamia miradi pamoja na ukusanyaji mapato. Yalio mema yaendelezeni na yale mabaya niliotenda yaacheni ,shirikianeni ,shikamaneni na mpeni ushirikiano Kiongozi mpya ili kuboresha ufanisi kazini .Mahali popote mikwaruzano haikosekani mimi ni binadam ,ninaondoka sina kinyongo na mtu yeyote kama kuna mtu nimemkosea basi naomba anisamehe Semwaiko alisema katika kuhitisha hotuba yake .
Kwa upande wa Wakuu wa Divisheni na Vitendo waliwakilishwa na Dkt.Ligonja ambae alipata kusema neno la shukrani kwa niaba ya Watumishi ,alisema wewe ulikuwa kiongozi mwema kwetu tumejifunza mengi kutoka kwako lakini pia sisi kama binadam tulikukwaza tusamehe na huko uendako Mungu akuongoze katika majukum yakomyko mapya .
Shabani K.Millao ambae ni mteule mpya katika nafasi ya ukurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi alimshukuru mtangulizi wake kwa kazi nzuri alioifanya ya kuisimamia Halmashauri na kumtakia yaliyo mema katika majukumu yake huko aendako. Akiongea na wakuu wa Divisheni na Vitengo Millao alisema ,leo siyo siku rasmi ya kuongea nanyi nitatafuta siku ya kuongea na watumishi ila niwaombe kushirikiana na kufanya kazi kwa bidii tuepuke majungu mahali pa kazi na badala yake tufanye kazi ya kuhudumia wananchi na kuawasililiza vyema wanapokuja na shida zao.Pamoja na hilo Millao alisisitiza ukusanyaji mapato na kusimamia miradi ili imalizike kwa wakati kama maagizo ya serikali yanavosema katika kutekeleza miradi na thamani ya pesa ionekane na si vinginevyo alisema mwisho wa kunukuu.
Katika picha Mustapha S Yusuff na Shabani K. Millao wakisaini Nyaraka za makabidhiano
Chanzo cha habari www.kondoadc.go.tz
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.