• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MAANDALIZI YA MSIMU MPYA WA KILIMO YATOLEWA KONDOA DC

Posted on: October 24th, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kupitia Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imeanza zoezi la utoaji wa elimu kwa wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa katika kuelekea msimu mpya wa kilimo.

Wakiwa kijiji cha Humai kata ya Soera, timu ya Wataalam kutoka Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Kampuni ya One Acre Fund wamejumuika pamoja na Wakulima na Wanakijiji  waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wakiwahamasisha kuhusu kanuni bora za kilimo kuelekea msimu mpya wa kilimo.

Akizungumza kwa njia ya mahojiano maalum Bi.Viasa Mpendu, ambaye ni Afisa Kilimo toka Divisheni husika, amesema "lengo la Mkutano huu ni kuwahamasisha wakulima juu ya kanuni bora za kilimo ikiwemo Upandaji kwa wakati wa mazao, matumizi ya viwatilifu, mbolea, kujisajili kwenye mfumo wa mbolea ya ruzuku, wakulima kuchangamkia huduma ya kupimiwa udongo kabla ya msimu wa kilimo kuanza, elimu ya Mifugo pamoja na kuwasogezea huduma ya uuzaji wa mbegu inayofanywa na kampuni ya One Acre Fund".

Kwa upande mwakilishi kutoka Kampuni ya One Acre Fund Ndg. Enhart Israel amesema wameanza kufanya majaribio ya kuwahudumia wakulima wa kanda ya kati (Dodoma na Singida) baada ya Nyanda za kusini kufanya vizuri, wakianzia Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa mkoa wa Dodoma na kukabidhi mbolea ya Chokaa kwa wakulima 86 kutoka kata za Soera, Salanka na Bereko lengo likiwa ni kupunguza tindikali kwenye udongo baada ya sampuli za udongo kupimwa na Halmashauri (awali) na sasa kuwauzia mbegu bora za mahindi, alizeti na maharage (Highbreed seed).

Kwa upande wao baadhi ya Wakulima walionufaika na elimu hiyo na Ununuzi wa mbegu waipongeza halmashauri kwa kuanza mapema zoezi la kuhamasisha wakulima kuhusu msimu mpya wa kilimo wakifurahia kusogezewa huduma ya kununua mbegu za mazao kilimo katika mashamba ya yao kwa gharama nafuu.

Zoezi hili la uhamasishaji wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ni zoezi endelevu katika kuelekea msimu mpya wa kilimo kutokana na jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta ya kilimo nchini kwa kuwawezesha maafisa ugani nchini vitendea kazi ikiwemo Pikipiki, Vishikwambi na Kipimia Udongo ambavyo Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imenufaika navyo.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.