• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

KONDOA DC YAPANIA UTOAJI WA CHAKULA MASHULENI KWA ASILIMIA 100

Posted on: August 14th, 2024

Wajumbe wa Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wamedhamiria kuhakikisha wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wanapatiwa Chakula mashuleni.

Hayo yamebainishwa katika kikao cha kamati ya lishe halmashauri mapema tarehe 13/08/2024 wakitathmini shughuli mbalimbali kupitia Divisheni za Elimu Awali,Msingi&Sekondari,Maendeleo ya Jamii, Kilimo,Mifugo &Uvuvi pamoja na Wadau wa Lishe wakilishwa na Chuo cha Madrasa cha Al-Madrasatul cha Masange.

Bi.Raiya Naser,kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amesema "suala la lishe ni suala endelevu na linabeba hatma ya Taifa,Mhe.Rais kwa kuliona hilo amesaini Mkataba wa utekelezaji na Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Mikoa wamesaini Mkataba na Wakuu wa Wilaya Mkataba wa utekelezaji wa lishe Bora kwenye maeneo yao ya Uongozi ".

Kwa kauli moja wajumbe wa kikao hicho walikubaliana kuwepo kwa Sheria ndogo za halmashauri ambazo zitasimamiwa na jamii husika wakihakikisha kuwa wazazi watakaokaidi kuchangia chakula shuleni kwa ajili ya watoto wao wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Akitilia mkazo juu ya sheria hiyo Bi.Line Chanafi ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari amesema lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanapatiwa chakula kwa 100%ngazi zote za elimu(Awali hadi Sekondari)itakayosaidia kuboresha kujifunza kwa watoto,kuboresha ufaulu,kupunguza na kumaliza utoro wa rejareja mashuleni.

"Katika kuimarisha Elimu ya kujitegemea mashuleni zaidi ya Tani 6,000 za mazao mchanganyiko yamevunwa kwenye mashamba ya Shule za Sekondari ikiongeza na kuboresha wigo wa utoaji wa chakula shuleni"alisema Bi.Chanafi.

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Bw.Juvenal Munishi amesema Maafisa ugani hushirikiana kwa karibu na wakuu wa shule katika kuendeleza Elimu ya kujitegemea mashuleni,wakitoa elimu stahiki ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kupata mazao na mifugo bora.

Kwa niaba ya Wadau wa Maendeleo eneo la lishe,Bw.Muadh Sungi ambaye ni mwakilishi kutoka Taasisi ya Madrasatul Ally-Badawi ya Masange alisema jamii ina kila sababu ya kupewa elimu ya lishe akitolea mfano kwenye kata yake ya Masange juu ya baadhi ya wananchi kwa kukosa uelewa juu ya umuhimu wa lishe akitaka jamii inayowazunguka kuiga mfano kutoka kwa kwao kwa kujishughulisha na ulimaji bustani za Mboga mboga na Ufugaji wa N'gombe na Mbuzi wa Maziwa kama sehemu ya Uchangiaji wa lishe kwenye jamii.

Hadi sasa ni asilimia 70 ya wanafunzi 42,075 kati ya wanafunzi 59,906 wa shule za msingi ndio wanaopata chakula,wengi wao ni madarasa ya mitihani (Darasa la 4 na 7)na kwa upande wa Sekondari wanaopata chakula ni 52.3%sawa na wanafunzi 5,396kati ya wanafunzi 10,322 wanapata huduma ya chakula shuleni.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.