• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

KONDOA DC YABEBA MAKOMBE MASHINDANO YA UMITASHUMTA 2024 MKOA WA DODOMA

Posted on: June 10th, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imeibuka kidedea kwa kubeba Makombe mawili, katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa kupitia mchezo wa Mpira wa Miguu (wavulana)na Mpira wa Pete (Wasichana).

Akiwapokea kwa shangwe, nderemo na bashasha jumla ya wanafunzi 92 kutoka mbali mbali za Msingi za halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Shaban Millao amewapongeza kwa kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano hayo na kuwataka kuongeza bidii zaidi katika mashindano yajayo.

Kwa Upande wake Afisa Michezo na Utamaduni Halmashauri Bw.Mohamed Chillo amesema mashindano hayo yalianzia ngazi ya shule, Kata, Kanda hadi ngazi ya wilaya ili kupata timu za michezo mbali mbali wapatao 92 ambao wameshiriki katika  mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa kwa kuibuka na ushindi katika fainali dhidi ya Chamwino (Mpira wa miguu) na ushindi dhidi ya Chemba (Mpira wa Pete).

Awali akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Elimu Awali & Msingi Bw.Eugen Shirima amesema mashindano hayo yamefanyika kwa muda wa siku nne, kuanzia tarehe 23-26 /05/2024 kwa kupata ushindi kwenye michezo ya mpira wa miguu na pete,mshindi wa pili kwenye riadha, mshindi wa tatu kwenye mchezo wa mpira wa mikono pamoja na kuchaguliwa kwa wanafunzi 14 kati ya 92 kujiunga kwenye timu ya mkoa ambayo itashiriki mashindano hayo kitaifa mkoani Tabora.

Pia kwa niaba ya timu ya wanafunzi hao Abdulhabi Ayubu kutoka Shule ya Msingi Hurui na  Asia Hassan kutoka Shule ya Msingi Madisa,  wamesema wamejiskia furaha kushiriki na kushinda kwa baadhi ya michezo walioshiri na kuahidi kuongeza bidii katika michezo wakizingatia fursa mbalimbali za michezo nchini.

Mashindano haya ya UMITASHUMTA na  UMISSETA kwa shule za Msingi na Sekondari kimkoa, yamefanyika katika shule ya Sekondari Dodoma yakizinduliwa rasmi na Katibu Tawala Mkoa Ndg.Kaspa Mmuya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.Rosemary Senyamule yakiwa ni mashindano ya 50 tangu kuanzishwa kwake nchini.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.