• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WAZIRI DKT. ASHATU AHIMIZA WELEDI NA UWAWAJIBIKAJI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KONDOA DC

Posted on: January 24th, 2026

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amewahimiza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuzingatia weledi, maadili ya kazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa lengo la kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

Dkt. Ashatu ameyasema hayo katika tafrija ya kuukaribisha mwaka 2026, iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Katika hotuba yake, Dkt. Ashatu, amewasisitiza watumishi kujenga utamaduni wa kuweka vipaumbele katika utoaji wa huduma bora, sambamba na kuendana na kasi na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuijenga Tanzania yenye maendeleo jumuishi katika sekta zote.

Aidha, Dkt. Ashatu amehimiza umuhimu wa upandaji miti na utunzaji wa mazingira kwa watumishi na wananchi kwa ujumla, ili kuendana na falsafa ya Tanzania ya Kijani.

Awali, akitoa salamu za Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kondoa, Ndg. Shaban Millao, amemshukuru Mhe. Dkt. Ashatu kwa kuhudhuria tafrija hiyo na kumpongeza kwa kuendelea kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupa Waziri kinara anayejitoa kwa dhati katika kuwatumikia wananchi. Sisi kama Halmashauri tuko pamoja naye na tunaendelea kutekeleza majukumu yetu kwa uadilifu na utu,” amesema Ndg. Millao.

Aidha, Ndg. Millao amemwomba Waziri Dkt. Ashatu Kijaji kumfikishia salamu za shukrani Mhe. Rais, kwa kuendelea kumuamini pia kwa Halmashauri kunufaika kwa kupokea watumishi wapya 222 wa kada mbalimbali, hatua itakayoongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Mhe. Salum Mabote, amesisitiza umuhimu wa umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa watumishi na viongozi wa wilaya katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Kondoa, Bi. Christina Kalekezi, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, amewataka watumishi kuzingatia maadili ya kazi na misingi ya utumishi wa umma kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, ili kujenga utumishi uliotukuka, wenye tija na unaolenga maslahi mapana ya Taifa.

Tafrija hiyo ilitanguliwa na Bonanza lililofana kwa kufanyika kwa michezo mbalimbali ambayo ilitoa fursa kwa Watumishi wote wa Halmashauri kushirikiana vyema, kuongeza upendo pamoja ukaribu zaidi

Matangazo

  • TANGAZO LA UKODISHAJI MAGARI October 16, 2025
  • MATOKEO KIDATO CHA SITA July 07, 2025
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE KONDOA DC YAPITIA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE

    January 26, 2026
  • WAZIRI DKT. ASHATU AHIMIZA WELEDI NA UWAWAJIBIKAJI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KONDOA DC

    January 24, 2026
  • KAMATI YA LISHE KONDOA DC YAFANYA ZIARA YA KIUTENDAJI

    January 22, 2026
  • MKURUGENZI MILLAO ASISITIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KONDOA DC

    January 20, 2026
  • Fungua zaidi

Video

Umeme kufika Kituo cha Afya Mauno-Kondoa:-Mkuu wa Mkoa Dodoma
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.