Leo tarehe 01/02/2022 halmashauri ya wilaya ya kondoa imefanya kikao chake cha baraza la madiwani cha robo ya pili kama ilivyo kawaida ya vikao vyake vya baraza la madiwani.Katika kikao hicho ambacho kimeanza majira ya saa tatu asubuhi kwa mh mwenyekiti wa halmashauri ndugu Abadallah Maguo kwa kuwakaribisha wageni mbali mbali walioalikwa katika kikao hiki ambao ni TARURA, RUASA ,TANESCO TFS na TTCL.Katika kikao hiki pia kilihudhuriwa na mh mkuu wa wilaya Dr, Mkanachi akiambatana na timu yake ya ulinzi na usalama. Baada ya ufunguzi mh mwenyekiti alimkaribisha meneja wa TARURA wilaya Eng Daud Sweke ili awasilishe taarifa yake kwa waheshimiwa madiwani inayohusiana na mtandao mzima wa barabara kondoa , baada ya kupewa fursa hiyo Eng sweke alieleza kwa kina jinsi ambavyo anatekeleza mipango yake katika kuboresha barabara pamoja na hilo pia meneja alisema kua changamoto zinazo rudisha nyuma juhudi hizi ikiwa ni pamoja na bajeti kutokutekelezwa kwa wakati maana alitengewa bilion 2.4 lakini hadi sasa kapokea milioni 800 peke yake lakini pia changamoto nyingine ni kuvunjika kwa kingo za mto kutokana na shuguli za kilimo , uharibifu wa barabara kutokana na mifugo na pia uhaba wa madini ya ujenzi japo tumezungukwa na milima. Baada ya maelezo yote ya kina madiwani walipata fursa ya kuuliza maswali yaliyolenga kutatua changamoto za barabara ikiwa ni pamoja na barabara ya cheke hadi filimo, barabara ya kikore hadi Araa , barabara ya bera bera Hanang barabara ya masange ,itololo hadi kisese pia daraja la kandaga na hurui. Majibu yaliyotolewa ilikua kama ifuatavyo daraja la kisese usanifu umekamilika na mkandarasi tayari yuko kazini pia barabara ya masange itololo hadi kisese mkandarasi yuko kazini japo wakati huu wa mvua ukarabati wa barabara unakua ni changamoto na daraja la kandaga linahiji kuwekewa kingo kitu ambacho aliahidi kukishughulikia maana liko ndani ya uwezo na barabara ya kwadelo mkandarasi tayari kapatikana.
Baada ya maelezo hayo kamati mbali mbali zilipata nafasi ya kuwasilisha taarifa zao kwani wakaribishwa wengine hawakuwepo , Kamati ya elimu afya na maji walifanya mwasilisho ,baada ya mawasilisho kipindi cha maswali kiliwadia ambapo mh mafita diwani wa kata ya changaa alitaka kufahamu ni upi mkakati wa halmashauri katika kukamilisha jengo la mama na mtoto katika zahanati ya chololo majibu yaliyotolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo diwani wa kata ya Itololo nikuwa tayari jambo hili limewekwa kwenye bajeti kwa utekelezaji.
Kamati iliyofuata ni kamati ya kudhibiti maambukizi ya ukimwi ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo alieleza kua tayari kuna vituo vitatu amabavyo vimekarabatiwa kwa ajaili yakutoa huduma ya tiba na ushauri nasaha ambavyo ni zahanati ya Chololo, Atta na kituo cha afya Mauno.Pia kamati ya ya uchumi ,ujenzi na mazingira waliwasilisha taarifa yao ambapo waheshimiwa walitaka kufaham ni lini majosho yatafanyiwa ukarabati ili iwe ni sehemu mojapo ya vyanzo vya mapato,jibu liliotolewa na afisa mifugo na uvuvi alisema tayari hatua za awali zimechukuliwa ikiwa pamoja na kufanya upembuzi kubaini ubovu wake na kwa kuanza wataanza na josho la bumbuta ndani ya mwezi huu. Kamati ya mwisho uwasilishaji taarifa ilikua kamati ya fedha,Uongozi na mipango ambapo ambayo ilieleza mambo mengi yanayohusiana na jinsi ambavyo halmashauri ianjipanga kuboresha mapato na pia iliulizwa vijiji vinavyozungukwa na minada vinanufaika na nini na kuwepo kwa vyanzo hivi? Majibu ilikua ni kwamba kila mnada unapofanyika basi kijiji husika hubaki na asilimia kumi ya mapato yake kwa ajili yakufanyia shughuli mbali mbali za maendeleo kama sehemu ya mapato yake.
Baada ya kamati zote kukamilisha mawasilisho yake mheshimiwa mkuu wa wilaya alipata nafasi ya kuhutubia baraza hili mh mkuu wa wilaya alisema lengo kuu ambalo madiwanai wanapaswa kulipa kipaumbele ni kuhakikisha suala la mapato linapewa kipaumbele nakuhakikisha sasa kiawango cha ukusanyaji mapato kinaongezeka na kutimiza malengo ambayo tumejipangia pia aliongeza na kusema kua madiwani wanapaswa kutimiza wajibu wao kama viongozi kwenye maeneo yao kwa kujibu kero mbali mbali kabla ya kero hizo kufika ngaazi za juu na pia washirikiane na wataalam mbalimbali waliyo kwenye kata zao katika kuharakisha maendeleo kwa wale wanao waongoza.Pia mwakilishi toka ofisi ya katibu tawala mkoa alisema tusimamie ukusanyaji mapato na kuziba mianya yoyote ambayo inaweza pelekea upotevu wa mapato pia kipaumbele kitolewe upande wa elimu ili kunyanyua kiwango cha ufaulu na kujikwamua na hali ambayo ipo kwa sasa na suala hili siyo la mtu mmoja mmoja bali ni watu wote kuanzia wazazi, walimu ,wanafunzi wenyewe pia wadau mbalimbali wa maendeleo.
Baada ya nasaha hizo toka wageni wakaribishwa mh,mwenyekiti alisimama kwa ajili ya kuahairisha baraza lakini na yeye pia aliendelea kusisitiza kua kipindi hiki tumejipanga kuhakikisha tunapandisha kiwango cha mapato ili kupata pesa za kutosha kwa ajili yakupeleka maendeleo kwa wananchi.Baada ya kusema hayo mwenyekiti aliahirisha kikao hadi wakati mwingine. habari na chanzo chetu www.kondoadc.go.tz
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.