• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

HALOTEL NA TRA WAKABIDHI MWADAWATI KONDOA-DC

Posted on: April 6th, 2019

Leo tarehe 06/04/2019 katika viwanja vya halmashauri ya wilaya ya kondoa kumefanyika hafla fupi ya kukabidhiana madawati yapatayo 55 yaliyotolewa na  kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi HALOTEL TANZANIA na mkurugenzi wa  kampuni  hiyo ndugu NGUYEN VEIN SON , Akikabidhi madawati hayo kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya kondoa ndugu Mstapha Semwaiko, mkurugenzi wa Halotel Tanzania aliambatana na Meneja wa Halotel mkoa wa Dodoma ndugu Duc Ha Minh pamoja na mkuu wa  mawasiliano na masoko ndugu Mhina Semwenda.

Wakati wa makabidhiano hayo ndugu Ngeyen alisema wao kama kampuni lengo lao ni kushirikiana na serikali katika kuboresha elimu na kuinua kiwango cha ufaulu  mashuleni pia alisisitiza kuwa kwa sasa halotel inatumia mfumo mpya unaoitwa  Halo study katika kujifunza ambapo mwanafunzi anaweza kujifunza elimu ya vitendo na kujisomea kupitia simu ya mkononi bila kuhitaji uwepo wa maabara au maktaba maana hivyo vitu vinapatikana kupitia mfumo wao mpya uliwekwa kwenye simu za mkononi.Aidha mkurugenzi huyo aliahidi kwa kusema kua atahakikisha huduma za mtandao wa halotel zinapatika kwa kondoa hasa maeneo ambayo hayana au yana mawasiliano ya kususua  na sehemu nyenginezo kama vile kata ya busi ,kata ya kinyasi ,kata ya keikei, kata ya pahi na sehemu nyinginezo ili kuchochea maendeleo.Baada ya kutoa shukrani zake kwa Mh. naibu waziri Dr,Ashatu Kijaji ndugu Nguyen alimwahidi mkurugnzi wa halmashauri ya kondoa kua atatoa simu za mkononi kwa maafisa wake wote hiinikiwa ni kuonesha mchango wa kampuni hiyo kwa taasisi yake.

Akipokea msaada huo mkurugenzi wa halmashauri  ya wilaya alimshukuru kampuni ya halotel kwa niaba ya wananchi wa halmashauri ya kondoa akisema msaada huu umekuja mda muafaka maana wanafunzi wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana walikua 705 na wanafunzi waliojiunga kidato cha kwanza mwaka huu ni jumla ya wanafunzi 3255 hali inayofanya kuwepo na upungufu mkubwa wa madawati ,aidha mkurugenzi aliendelea kumwomba mkurugenzi wa kampun hiyo kua wasichoke kuendelea kutusaidia kwani wao ndiyo wadau wakubwa wa maendeleo,na alihahidi kujenga mahusiano baina  yao kwa maendeleo ya nchi. Vilevile  ndg semwaiko alimshukuru naibu waziri fedha mh Dr kijaji kwa juhudi zake za kuinua kiwango cha elimu na maendeleo wilaya ya kondoa kwani vipaumbele vyake ni vitatu namba moja elimu,namba mbili elimu na namba tatu elimu. 

Akitoa ufafanunzi wa mgawanyo wa madawati hayo ndg  Semwaiko alisema madawati  yatagawanywa kama ifutavyo  sekondari ya busi madawati 15,sekondari ya Bumbuta 15,sekondari ya Imbafi 10 na sekondari ya Kalamba 15.

Katika tukio lingine lililofanyika siku ya leo katika ukumbi wa kondoa irangi, tumeshuhudia naibu waziri wa fedha na mbunge wa kondoa Mh Dr Ashatu Kijaji akikabidhi mawadati yapatayo 100 kwa mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya kondoa ikiwa ni miongoni mwa ahadi zake za kuendelea kuboresha kiwango cha elimu kwa kuweka miundombinu bora ya kujifunzia hii ikiwa ni moja ya kauli mbiu yake ya kwamba" aliahidi na anatekeleza" na haya yote yamefanyika ndani ya miaka mitatu tu ya uongozi wake.

Akikabidhi madawati hayo mh waziri alisema madawati haya aliyapata ikiwa ni msaada kutoka TRA baada juhudi zake binafsi ili kutimiza kile ambacho kitaleta manufaa katika kuleta maendeleo na kuijenga kondoa mpya.Alisema upungufu ni mkubwa kutokana na idadi kubwa ya watoto wanaojiunga na kidato cha kwanza lakini akasisitiza kua ifikapo 2020 lazima tuwe tumefikia lengo na kumaliza tatizo hili la upungufu wa madawati katika shule zetu.

Wakati wa makabidhiano ya madawati hayo mh mbunge aliambatana na mwenyekti wa CCM wilaya mh Gora ,Makamu mwenyekiti wa halmashauri mh Hija Sulu na Katibu wa CCM wilaya ambao kwa pamoja walishukuru jitihada za mh mbunge katika kuipigania kondoa mpya na kusema hawakukosea katika kumchagua na kupeperusha bendera ya chama tawala. 

                                                                                               















                                                                                   









.

  


Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.