• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Wazindua Utoaji Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto Chini ya Miaka Mitano

Posted on: March 15th, 2019

Zoezi la usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano lazinduliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kata ya mnenia kijiji cha itundwi ,ambapo mgeni rasmi akiwa mwenyekiti wa halmashauri mhe. Gaspar mwenda.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg. Mustapha Semwaiko Yussuf wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi,aliwasihi wananchi wote wenye watoto wa umri  chhini ya miaka mitano kutumia fursa hii ya kuwa na vyeti vya kuzaliwa watoto bila gharama yoyote ili kuwaepushia usumbufu wa kuvipata kipindi wakivihitaji.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Kondoa akiongea na wananchi wa kijiji cha Itundwi

Wakati akitoa hotuba ,mgeni rasmi aliwakumbusha wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya kondoa juu ya umuhimu wa mtoto kuwa na cheti cha kuzaliwa kwani kinatumika kama utambulisho wa kwanza wa mtoto,lakini pia ni muhimu kwa mtoto kipindi akihitaji huduma ya elimu katika ngazi zote.zaidi ya yote Cheti cha kuzaliwa ni haki ya mototo.

Mgeni Rasmi mhe.Gaspar mwenda(Mwenyekiti wa Halmashauri) akitoa hotuba wakati wa uzinduzi.

Zoezi hili limetanguliwa na mafunzo kwa maafisa usajili wasaidizi mia moja ishirini na tatu(123) kutoka kata zote ndani ya Halmashauri na huduma zinatolewa katika vituo vya usajili ambavyo ni ofisi za watendaji wa kata na vituo vya kutolea huduma za tiba(zahanati,vituo vya afya na Hospitali) ambapo jumla ya zaidi ya watoto 33000 wanatarajiwa kusajili ndani ya wiki mbili.

Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi mtendaji(W) Ndg. Mustapha Semwaiko Yussuf(wa pili toka kushoto chini) na wasajili wasaidizi pamoja na wawezeshaji wa mafunzo

Ili mtoto aweze sajiliwa na kupatiwa cheti cha kuzaliwa,mama na/au baba wanapaswa kufika na kadi ya kliniki na tangazo la kizazi. Iwapo mzazi hatakuwa na vyote viwili,basi atapaswa kufika na barua ya utambulisho toka kwa mtendaji wa kijiji.

Awali wawakilishi toka wakala wa usajili ufilisi na udhamini(RITA) walifafanua lengo la Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha watoto wote chini ya miaka mitano wanapatiwa  vyeti vya kuzaliwa bure litakuwa ni endelevu ambapo kwa kuanza katika halmashauri usajili wa watoto thelathini na tatu elfu utafanyika.

Wasajili toka RITA wakiwasalimia wananchi na kusisitiza jambo wakati wa uzinduzi eneo la Itundwi kata ya Mnenia.

Mwenyekiti alizindua zoezi kwa kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa baadhi ya watoto na wazazi waliofika kupata huduma.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 12, 2025
  • RC SENYAMULE AFANYA ZIARA KONDOA DC

    May 13, 2025
  • ELIMU YA UZUIAJI UPOTEVU WA NAFAKA KUWA SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA KONDOA DC

    May 11, 2025
  • WANANCHI KIJIJI CHA ITUNDWI WAADHIMISHA KWA VITENDO SIKU YA AFYA NA LISHE

    May 07, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.