HALMASHAURI YA WILAYA KONDOA YAPOKEA HATI
Halmashauri ya wilaya Kondoa imepata hati safi kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali baada ya Taarifa ya fedha 2021/2022 kupata hati inayoridhisha kupitia jumla ya hoja za ukaguzi 51.
Katika taarifa yake Kwenye kikao Maalum cha Baraza la madiwani hapo jana tarehe 11.07.2023 Ndg Chambi Sasamka ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Nje Hesabu za Serikali Mkoa wa Dodoma amesema ‘’ Kwa taarifa ya mwaka 2021 /22 Halmashauri ya Wilaya Kondoa ilipata hati inayoridhisha na mwaka huo halmashauri ilikua na jumla hoja za ukaguzi 51 zikijumisha hoja 19 za miaka ya nyuma baada ya taarifa ya ukaguzi huo kutolewa ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu Dodoma ilipokea taarifa ya utekelezaji tar 19.05.2023 na kwa kushirikiana na Wataalam wa Halmashauri kwa kufanya Uhakiki.‘’.
Ndg Chambi amesema baada ya uhakiki hoja 18 zimepatiwa majibu ya kuridhiwa kufungwa na kusalia hoja 33 sawa na 65% ya hoja zote.Vivyo hivyo amebainisha baadhi ya hoja zilizojitokeza katika ukaguzi wa mwaka 2021/2022 ni pamoja na shule mpya ya sekondari keikei ambayo haijakamilika kutokana na uhaba wa fedha sh mil 163,329,559, kuuchelewa kukamilika ujenzi kwa jengo la Makao Makuu ya Halmashauri, Mabweni ya Wanafunzi yenye thamani ya sh Mil 150.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule amesema‘’Hati hii safi inaipa heshima Wilaya ya Kondoa ,Mkoa wa Dodoma na Nchi kwa ujumla wake, mafanikio haya kwa ujumla yanatokana na ushirikiano chanya baina ya Watumishi wa Halmashauri, Viongozi Madiwani na Wadau mbalimbali hivyo nawasihi endeleeni kudumisha ushirikiano huu ili kuiwezesha halmashauri ya wilaya kondoa kuendelea kupata hati safi katika kaguzi zote kila mwaka’’.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt khamis Mkanachi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya Kondoa kwa kuzipunguza hoja zilizowasilishwa na Mkaguzi wa Serikali vivyo hivyo pongezi kwa Ofisi ya Mkaguzi wa Hesbu kwa kuibua hoja na kusema ‘’ukaguzi wa CAG hauji kwa kushtukiza ,ni jambo la kisheria kwa kalenda maalum na tunapaswa kujitahidi kwenye eneo la kuweka Nyaraka sawasawa ,ili hoja zinapokuja zijibiwe vizuri’’
Akihitimisha kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Mohamed Maguo amemshukuru Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa kuweka wazi maswala ya Fedha na Miradi katika halmashauri yao na kumuomba mkaguzi kuendelea kuwakagua kwa Maendeleo ya Halmashauri pamoja na kuahidi kutimiza maelekezo yaliyotolewa na viongozi wa Wilaya na Mkoa katika kikao hicho cha baraza maalum la kujadili taarifa za hoja zilizoibuliwa na mkaguzi wa hesabu za serikali .
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.