• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DC NYANGASSA ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KATA YA KISESE-KONDOA DC

Posted on: August 1st, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Fatma Almas Nyangassa amefanya  Ukaguzi wa Utekelezaji wa Mradi wa Maji Kisese Sauna wenye thamani ya Tsh Mil 913 pamoja na kusikiliza kero za wananchi kata ya Kisese.

Mhe.Nyangassa amefanikiwa kukagua Chanzo cha Maji kitakachowanufaisha wananchi baada ya Mradi kukamilika, alishuhudia maendeleo ya mradi ulipofikia na kuagiza kuongeza kasi ya ukamilishaji mradi kwa wakati na ubora hadi kufikia tarehe 30/09/2024 mradi uwe umekamilika.

Akiwa kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa kata hiyo  Mhe.Nyangassa amesikiliza na kutatua kero zinazowakumba wananchi hao zikiwemo za sekta ya Maji, Afya,TASAF na Barabara akiahidi kuzifanyia kazi.

Mhe.Nyangassa amesisitiza ushirikiano baina ya Jamii na Viongozi kwa maendeleo ya Kondoa, wananchi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wakazi (Uchaguzi wa Serikali za Mitaa) na Daftari la kudumu la Wapiga kura (Uchaguzi Mkuu mwaka 2025) pamoja na Upingaji Ukatili wa Kijinsia dhidi ya watoto na wazee.

Kwa upande wake Diwani mwenyeji, Mhe.Abubakari Maleda amempongeza Mhe.Nyangassa kwa kufika kusikiliza na kutatua kero kwenye kata yake akielezea tumaini lake juu maelekezo aliyoyatoa kwa uongozi wa RUWASA-KONDOA na Mkandarasi wa Mradi wa Maji kwenye kata hiyo.

Mradi wa Maji Kisese Sauna unatekelezwa na Mkandarasi aitwae TS SOLUTION LTD na hadi sasa mradi umetekelezwa kwa asilimia 77 ya mradi ikijumuisha Ujenzi wa Dakio (Intake), Ukarabati wa Tanki la Maji lenye uwezo wa ujazo wa lita 35,000,Ujenzi wa Nyumba ya Mlinzi, Ujenzi wa Tanki la Maji la lita 75,000, Ujenzi wa Vituo vya Maji 15, Ujenzi wa Malambo 2, Ujenzi wa Ofisi  CWBSO pamoja na ulazaji wa Bomba la kusambazia maji Mita 18,544.

Mradi huu unalenga kuwanufaisha jumla ya wakazi 6,642 wa vijiji vya Kisese Sauna na Mapinduzi kwa kutatua adha ya maji inayowakumba wananchi hao kwa muda mrefu wakifuata maji katika vijiji jirani.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.