• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

CHMT KONDOA DC YANG'ARA KATIKA USIMAMIZI WA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

Posted on: March 3rd, 2025

Timu ya Halmashauri ya Uendeshaji wa Huduma za Afya (CHMT)Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imepongezwa kwa kufanya vizuri katika usimamizi wa huduma za afya.

Pongezi hizo zimetolewa na Ujumbe kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii OR-TAMISEMI ukiongozwa na Dkt.Rashid Mfaume alipotembelea na kukagua huduma za afya, lishe na ustawi wa jamii katika Halmashauri hiyo.

"Niwapongeze kwa utayari wenu wa kutoa huduma bora kwa wananchi, nimeridhishwa na bidii yenu ya usimamizi wa miradi inayoendelea hapa (Ujenzi wa Jengo la Upasuaji, Wodi ya Upasuaji ya Wanaume na Wanawake  n.k) nguvu kazi iliyopo inaonyesha ni kwa namna gani kazi zinafanyika usiku na mchana kwa kufunga taa maeneo ujenzi unakoendelea "amesema Dkt.Mfaume.

Kwa niaba ya watumishi hao  wa afya Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri, Dkt.Ernest Msemakweli ameushukuru ujumbe huo kwa pongezi hizo akiahidi kupokea ushauri uliotolewa na ujumbe huo kwa maslahi mapana ya afya kwa jamii.

Sambamba na pongezi hizo Ujumbe huo uliwazawadia watumishi hao kiasi cha Tzs 158,000 ambacho

 kilipokelewa na Mganga Mfawidhi Hospitali ya Halmashauri iliyopo Bukulu Dkt.Alpha Kwilasa kama motisha kwa watumishi hao kutokana na kuridhishwa na utoaji wa huduma za afya katika vituo walivyotembelea.

Miongoni mwa vitu vilivyowavutia ujumbe huo ni pamoja na uwepo wa Picha za kuvutia zenye jumbe elezi kwa watoto na lishe katika wodi yao ambazo husaidia wananchi  na wagonjwa kupata elimu moja kwa moja kitu ambacho ni nadra katika hospitali nyingi nchini, Upatikanaji wa dawa kwa 96% ununuzi wake ukifuata miongozo,mpangilio mzuri,uhuishwaji wa taarifa za dawa kwa wakati,uwepo wa jokofu na ubaridi unaoridhisha Chumba cha Dawa katika hospitali hiyo.

Ziara hiyo ya ukaguzi wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa jamii inalenga kuwajengea uwezo na weledi wataalam wa afya katika Mkoa wa Dodoma ikiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, ujumbe huo umetembelea na kukagua huduma za afya, lishe na ustawi wa jamii zinazotolewa katika Hospitali ya Halmashauri iliyopo Bukulu na Kituo cha Afya Bereko

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.