• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

BARAZA LA MADIWANI LAMPONGEZA MKUU WA DIVISHENI YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KONDOA DC

Posted on: August 27th, 2024

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa limempongeza Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw.Juvenal Anthony Munishi kwa kusimamia vyema ushiriki wa Halmashauri katika maadhimisho ya wakulima NANE NANE Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nzuguni Dodoma kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti 2024.

Hiyo ni baada ya Halmashauri kushiriki  Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima NANE NANE kwa muda wa siku 8 na kuibuka mshindi wa maonesho hayo kwa nafasi ya pili kati ya Halmashauri 8 za Mkoa wa Dodoma.

Akitoa pongezi na kumkabidhi zawadi kwa niaba ya Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Abdalah Maguo amesema kwa watumishi wengine watakaofanya vizuri wazawadiwe vivyo hivyo na hata kwaWaheshimiwa Madiwani watakaofanya vizuri katika kata zao kwenye usimamizi mzuri wa miradi ya  maendeleo pia wazawadiwe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao amesema utoaji wa pongezi kwa mkuu wa Divisheni hiyo ikawe chachu kwa wakuu wengine wa divisheni na vitengo na watumishi wengine katika kufanya kazi kwa ufanisi ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Pia Ndg.Millao ameongeza pamoja na halmashauri kupokea tuzo iliyotolewa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kilele cha maonesho ya Wakulima NANE NANE Kimataifa yaliyofanyika viwanja vya Dodoma, uongozi wa Halmashauri umemzawadia cheti cha pongezi na fedha taslimu Sh.Mil 1  Ndg.Juvenal Anthony Munishi kama motisha kutokana na juhudi zake.

Kwa upande wake Ndg.Juvenal Munishi  ametoa shukrani za dhati kwaBaraza la Madiwani kwa kutambua mchango wa Divisheni hiyo, wakiwatia chachu katika ufanyaji  kazi,akishukuru Jitihada za Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi kwa maafisa ugani na kuahidi kuongeza bidii ya kuwasaidia wakulima na Wafugaji wa Kondoa.

Sambamba na hilo katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani Robo ya Nne kamati za kudumu za halmashauri ziliwasilisha taarifa za utekelezaji wa  shughuli mbalimbali za maendeleo ya Halmashauri kwa kipindi cha robo ya nne mwaka wa fedha 2023/2024.

Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wamekuwa wakifanya vyema kwa kupokea teknolojia mbalimbali na elimu kuhusu matumizi sahihi ya viatilifu na mbolea kupitia Maafisa Ugani wakileta mabadiliko chanya ya matumizi ya kanuni xa kilimo bora ikiwemo matumizi ya mbolea za viwandani kutoka Tani 320.6 kwa mwaka 2022/2023 hadi Tani 619.5 mwaka 2023/2024.

 Mazao yanayolimwa kwa wingi  Halmashaur ya Wilaya ya Kondoa ni pamoja na Mahindi, Mtama, Uwele, Mbaazi, Dengu, Ufuta na choroko.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.