Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Kondoa limemkaribisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Halmashari ya Wilaya ya Kondoa Ndg Shabani ikiwa ni baada ya Teuzi mpya zilizofanywa na Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Wakurugenzi nchi nzima siku chache zilizopita
Akimtambulisha mbele ya Baraza la madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Mohamed Maguo amesema katika halmashauri yao mabadiliko yamefanyika kwa nafasi ukurungenzi nchini baada ya Mh, Rais Samia kumteua ndg shaban Millao kuwa Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya wilaya Kondoa kwa kuchukua nafasi ya ndg Mustapha Semwaiko ambaye amepangiwa majukumu mengine na serikali na kuwaomba waheshimiwa madiwani kufanya nae kazi kwa kipindi chote atakachodumu nafasi yake ya ukurugenzi baaada kuteuliwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi mpya Ndg Shabani Millao amesma anaamini kwa pamoja katika ushirikiano uwezo wa kuifikisha Halmashauri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kutekeleza azma ya mheshimiwa Rais ya kuwaondoa watu kwenye umaskini kutoka hatua moja hadi nyingine na kuwaaidi waheshimiwa Madiwani kufika kwenye kata zao kwa utambulisho Zaidi.
Pia kwa kwa upande wa waheshimiwa madiwani wa kata zote ndani ya Halmashauuri ya wilaya Kondoa wakapata nafasi ya kujitambulisha kila mmoja katika kata wanazozihudumu
Ndgu Shaban Millao kabla ya kuteuliwa na Mheshiwa Rais kwa nafasi ya Ukurugenzi Halmasha ya Wilaya ya Kondoa amehudumu katika halmashauri mbalmbali kwa nafasi ya Afisa mipango ikiwemo Halmashari ya Mpwapwa pamoja na halmashauri ya Chalinze wilayani babamoyo ambayo amedumu katika nafasi ya afisa mipango kwa miaka 12.
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.