• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

BAJETI ZA HALMASHAURI MWAKA 2019/2020 KUHAKIKISHA ZINA AFUA ZA LISHE :TAMISEMI

Posted on: November 23rd, 2018

Ofisi ya Rais-TAMISEMI wameendesha mafunzo ya siku moja katika Wilaya ya Kondoa ikijumuisha wajumbe wa kamati za lishe katika Halmashauri mbili ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Halmashauri ya Mji wa Kondoa.Wajumbe  walikuwa Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kondoa,Katibu tawala Wilaya,Wenyeviti wa Halmashauri zote mbili,wakurugenzi wa Halmashauri zote,wakuu wa idara na Vitengo.Katika mafunzo hayo wawezeshaji walikuwa Bw.Madaha Malekela(OR-TAMISEMI),Bi.Marian Mwita(Afisa Lishe Mkoa) na Bi Doroth Msimbila(Shirika la Konsonanti) wakishirikiana na wenyeji wao Bi. Evelyne Kabitina,Afisa lishe Halmashauri ya Wilaya-Kondoa na Bi. Dorice Munisi,Afisa lishe Halmashauri ya Mji-Kondoa.Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.


Katika ufunguzi wa mafunzo Mkuu wa Wilaya Bi Sezaria V. Makota aliwataka washiriki kuwa wasikivu na kuyazingatia mafunzo kwani mafunzo hayo ni muhimu kwa mustakabali wa jamii ya Kondoa na watanzania kwa ujumla wake.Hii ni kutokana na ukweli kwamba malezi ya watoto kwa kuwapa lishe bora unachangia kwa kiasi kikubwa katika  ukuaji wa mtoto kiakili.

Wakati Bi Doroth Msimbila alipokuwa akiwasilisha mada  ihusianayo na mpango mkakati wa utekelezaji,amefafanua maana halisi ya  lishe kuwa ni  mchakato wa tangu chakula kinapoliwa mdomoni, kinasagwa na kuingia mwilini na kuainisha madhara ayapatayo mtoto anapokosa lishe bora kuwa ni  kupata upungufu wa madini na Vitamini mwilini.Wawezeshaji wote kwa pamoja wamesisitiza juu ya kumuhudumia mtoto katika siku 1000 za kwanza kwani ndio kipindi ambacho ubongo wa mtoto unatengamaa.Hiki ni kipindi kinachoanzia kutungwa kwa mimba hadi umri wa miaka miwili. Kila mara mama au baba anapocheza na kucheka, kusoma kitabu au kushiriki mchezo na mwanawe, ujue kuna maelfu ya hisia chanya zinazojengeka kwenye ubongo wa mtoto huyo mchanga, zinazojenga uwezo wake wa kujifunza, utendaji, kuendana na mabadiliko na hata kukabiliana na changamoto.


Wakati wa kupitisha wajumbe katika uandaaji wa bajeti ya Afya kupitia mfumo wa Planrep,Bw. Madaha amewajulisha wajumbe kuwa Ili kuweza kufanikisha katika kuhakikisha Watanzania wanapata elimu juu ya  Lishe Bora,Serikali imeamua kwamba kwa Halmashauri zote nchini zinapaswa kupanga na kusimamia utekelezaji wa bajeti ya Afya katika afua za Lishe kwa kuzingatia takwimu sahihi za idadi ya watoto chini ya miaka mitano(05) katika wilaya husika.

Wenyeviti wa Halmashauri zote mbili wameshukuru kwa kupata Elimu ya Lishe ambayo kimsingi hawakuwa wanaifahamu kabla ya mafunzo.Wamewataka

Maafisa Lishe Wilaya Kuwashirikisha katika vikao  vinavyohusu lishe bila kujali vinamalipo au havina malipo ili wao kama wawakilishi wa wananchi waweze kuwajulisha wananchi wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Pia imeshauriwa kuifanya ajenda ya Lishe kuwa ajenda ya kudumu kwa viongozi wote wa wilaya ili kuiwasilisha kwa wananchi wakati wowote wanapopata fursa ya kuongea na wananchi au viongozi wa kata au vijiji/mitaa ili kuongeza ufahamu zaidi kwa wananchi juu ya masuala ya lishe bora.

Wakati wa kuhitimisha,washiriki kutoka Halmashauri zote waliweza kuweka mipango ya kutekeleza(way forward) ili kuweza kufikia lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya Lishe.

HABARI PICHA

Wawezeshaji wakiwa makini kusikiliza maswali toka kwa wajumbe.

Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa wakati akizungumza hasa juu ya kushirikishwa katika vikao vya lishe.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.


Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.