Kamati ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa Mkoani Dodoma (ALAT) imefanya ziara yakeHalmashari ya Wilaya ya Kondoa Tarehe2.07.2023 katika vijiji vya Haubi ,Bukulu na Poteakwa kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Ndg Isaack Luambano ambaye ni Mratibu mradi LDFS-KONDOA amesema lengo la Mradi nikurejesha Ardhi iliyoharibika ,kuongeza Uzalishaji wa chakula pamoja na kuboresha Uchumiwa wanufaika kwa kutumia Teknolojia ya Mbegu 9 na jembe la Mzambia ambazozimetumika katika Kilimo cha Mahindi ndani ya vijiji vya Haubi na Mafai.
Kupitia Ujenzi wa vyumba 7 vya Madarasa na Matundu 3 ya vyoo Shule ya msingi Potea NdgSelemani Yange Said ambaye ni Mwalimu mkuu amesema hadi kufikia June 30 2023 Ujenziwa vyumba 03 vya Madarasa umekamilika,Ujenzi wa vyumba 04 vya Madarasa upo katikahatua ya Upauaji na Upakaji rangi pamoja na ujenzi wa matundu 8 ya vyoo upo katika hatuaya kuinua ukuta Ikiwa jumla ya sh mil241,025,500 za serikali kuu n ash 62,380,115zilikuazimeshatumika kwa ajili ya ununuzi wa wa vifaa vya ujenzi pamoja na malipo yamafundi.
Kwa upande wake Dr alpha kwilasa ambaye ni Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya Kondoaamesema huduma zitolewazo ni huduma za Wagonjwa wa nje(OPD),Huduma ya kujifungua,hudum ya mama,baba na mtoto ( RCH) ,Huduma za Maabara,huduma ya Kinywa na Meno,Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma pamoja na Huduma zinginezo zilzochangia mafanikio yajumla ya wakina mama 122 wamejifungua salama ,Huduma kwa wateja wa OPD4,055,Huduma ya Outreach kwenye vijiji 4,nyongeza ya idadi ya watumishi,ukamilikaji wanyumba ya watumishi (3in 1) ,kuanza kwa huduma ya mionzi ambapo hadi sasa wateja 133wamenufaika na huduma hii pamoja upatikani wa gene xpert ambapo hadi sasa wateja2,283 wamenufaika.
Akihitimisha ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati ya ALAT mkoa Ndg. White Zuberi amesemawamefurahia Teknolojia ya kilimo hiko cha kisasa na kuaidi kwenda kufanya katikaHalmashauri zao maana changamoto za udongo zinafanana kwa kuwa na ardhi yenye kichanga na upungufu wa mvua .
Aidha katika utekelezaji wa Miradi kijiji cha Potea na bukulu Mh Zuberi White amempongezaMkurugenzi mtendaji wa halmashauri na Watumishi kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyoiliyopo kwenye hatua mbalimbali za ukamishaji.Habari na chanzo chetu www.kondoadc.go.tz,
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.