Halmashauri ya wilaya ya Kondoa leo tarehe 21 mwezi wa sita imesaini mradi wa ujenzi wa maji Kijiji cha Haire Katika kata ya Itaswi.Katika zoezi hilo ambalo uwekaji sahihi umefanyika ofisi ya Mkurungezi wilaya ya kondoa ,upande wa Halmashauri umewakilishwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Mh, Gasper Mwenda ,Kaimu mkurugenzi ndugu Mashauri Msimu ,Kaimu afisa mipango Joshua Mnyang'ali na Mhandisi wa maji eng. Falaura, na upande wa kampuni ya NYAKIRE INVESTMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM ambayo ndo mjenzi wa mradi huo umewakilishwa na eng, PASCAL ANDREW ambae ndo msimamizi wa mradi huo.Nikiongea na mhandisi wa mradi huu amesema mradi unagharimu kiasi cha fedha zipatazo milioni 383,244,988 ikiwa ni fedha toka serikalini pia amesema mradi huu unategemewa kukamilika ndani ya miezi tisa kuanzia sasa .Pia Mh Mwenda alisema anashukuru sana serikali kwa kuleta mradi huu maana utaenda kutatua tatizo la uhaba wa maji linalowakabili wananchi wa kijiji hiki cha haire na kusisitiza kua kama masharti ya mradi yanavosema kua utakamilka ndani ya miezi tisa,ukamilike kwa wakati ili kuwaondolea adha ya maji wananchi wakiji hiki.Pia kaimu mkurugenzi wa halmashauri ndugu Mashauri baada ya kutiliana sahihi alisema mradi utekelezwe kwa kufuata vigezo vyote vya kitaalam kama ilivyo ainishwa kwenye mkataba ili kuleta ufanisi na ubora katika mradi huo.
katika picha ni mhandisi wa maji eng, Falaura akitoa maelekezo wakati wa utilianaji sahihi na mhandisi wa kampuni ya Nyakire Investment ndugu Pascal Andrew.
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,KILIMANI STREET
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.