• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

ZAIDI YA MILIONI 90 ZATOLEWA KWA VIKUNDI VYA WAJASILIAMALI KONDOA DC

Posted on: October 31st, 2024

 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kupitia Kitengo cha Maendeleo ya Jamii imekabidhi jumla ya Sh.96,070,000 kwa Vikundi 7 vya wajasiliamali ikijumuisha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Akikabidhi hundi ya mfano ya malipo kwa vikundi hivyo mgeni rasmi wa hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Fatma Nyangassa amempongeza Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu uendelezwaji wa kutoa mikopo ya 10% baada marekebisho muhimu kufanyika  ambayo awali ilisitishwa.

"Sisi kama viongozi tuna kazi kubwa ya kuwaelimisha wananchi wetu juu ya mikopo hii tukijiridhisha kwa kupata taarifa sahihi zinazohitajika kwa waombaji wa mikopo ili watu wengi zaidi wanufaike nayo kama ilivyo dhamira ya Mhe.Rais ya kuwezesha watanzania wengi katika masala ya kiuchumi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Abdalah Maguo ameviasa vikundi hivyo kuzitumia fedha kikamilifu katika vikundi vyao na kufanya marejesho kwa wakati ili na vikundi vingine vipya vinufaike.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg.Shaban Millao amesema,  Halmashauri ya wilaya ya kondoa imejipanga kuhakikisha uchumi wa wananchi wake unaimarika ukiwazingatia vijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalum kupitia njia mojawapo ya mikopo ambapo kiasi cha fedha Sh 222,398,512.35 zimetengwa kama sehemu ya 10%ya mapato ya ndani zilizoanza kutengwa tangu mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Awali katika taarifa yake Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri Bi.Raiya Nasser amesema mikopo hiyo ilisitishwa na Serikali mwezi April 2023 na kupewa idhini ya kuendelea nchini mwezi Septemba 2024 ikihimiza  uhamasishaji wananchi kuanza kuomba mikopo katika  halmashauri, huku vikundi 7 vikikidhi vigezo vyote  muhimu na kuwapa mafunzo toshelevu dhidi ya usimamizi bora wa miradi yao, uwekaji akiba n.k.

Kwa upande wa vikundi vilivyopata mkopo huo  wamemshukuru Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia zoezi la utoaji mikopo kuendelea, wakiahidi kuzitumia kwa malengo husika na kuhakikisha wanarejasha kwa wakati.

Vikundi vilivyonufaika na mkopo huo kwa dirisha la kwanza ni pamoja na Vikundi vya Wanawake (Matumaini-Itololo, Mtakuja-Kikilo,Tanzanite-Haubi),Vijana (Uhakika-Bereko,Vijana Electronics-Kisese) Watu wenye Ulemavu (Watu wenye Ulemavu JKwadelo, Nyota-Mnenia).

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.