• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WATAALAM WA ELIMU KONDOA DC WAPIGWA MSASA KWA VITENDO ELIMU YA UOTESHAJI MICHE YA MITI

Posted on: July 12th, 2025

Wataalam wa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wamejengewa uwezo juu ya uoteshaji wa miti ya matunda na kivuli kwa vitendo.

Mafunzo hayo yamefanyika  katika Chuo cha Ualimu Bustani yakiwakutanisha Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wa shule za msingi halmashari yakiongozwa na Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira.

Akiendesha mafunzo hayo Afisa Misitu Halmashauri Ndg.Clement Kabeni amesema kuna faida nyingi tunazipata kwa kuotesha na kutunza miti ya kivuli na matunda,akiwafundisha wataalam hao namna bora ya upandaji na utunzaji wa miti ya matunda ya muda mfupi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mapokezi ya miti hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Msingi Mwl.Eugen Shirima amekipongeza kitengo cha Maliasili na hifadhi ya Mazingira kwa elimu walioitoa kwa wataalamu hao,akiahidi utekelezaji wake katika shule zote za msingi ambapo siku chache zijazo zoezi la usambazaji wa  miche ya miti ya matunda 100 kwa kila shule litaanza.

" Kupitia mradi wa Shule Bora katika Halmashauri yetu,shule zetu za Msingi zitanufaika kwa kupewa miti ya matunda 100 kwa kila Shule ambapo hadi sasa taratibu za manunuzi zimefanyika katika chuo cha Sokoine-Morogoro, nielekeze kwenu wataalam wa elimu kuhakikisha mnaitunza miti hiyo itakapofika kwenye shule zetu sambamba na uzingatiaji wa elimu ya upandaji Miti tuliyoipata leo"alisema Mwl.Shirima.

Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imejiwekea mkakati madhubuti wa kuhakikisha taasisi zote za umma zinatekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Sita chini Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe kwa watoto mashuleni kwa upandaji na utunzaji wa miti ya matunda.

Sanjari na mikakati hiyo halmashauri imeanzisha vitalu mbalimbali vya miche ya matunda na kivuli vilivyopo katika viwanja vya jengo la utawala pamoja na ushirikiano madhubuti na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS-Kondoa),Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Inades Formation Tanzania na Green Africa katika kuhakikisha Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa inakijanishwa kwa utunzaji wa mazingira ikiwa zaidi ya miti Elfu 37 imepandwa.

Matangazo

  • MATOKEO KIDATO CHA SITA July 07, 2025
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WANOLEWA MFUMO WA E-UTENDAJI

    July 12, 2025
  • KONDOA DC YAJIPAMBANUA UFAULU MATOKEO YA MOCK MKOA 2025

    July 12, 2025
  • WATAALAM WA ELIMU KONDOA DC WAPIGWA MSASA KWA VITENDO ELIMU YA UOTESHAJI MICHE YA MITI

    July 12, 2025
  • ZAIDI YA WATU 14,000 KUNUFAIKA NA MRADI MKUBWA WA MAJI KWADELO

    July 01, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.