• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

"WANAWAKE WENZANGU JITOKEZENI KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MWAKA 2024" RC ROSEMARY SENYAMULE

Posted on: August 28th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amewataka wanawake nchini kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Mhe.Senyamule ameyasema hayo alipokua katika Uzinduzi wa Tamasha la Saba la Jinsia ngazi ya Wilaya-Viwanja vya Sabasaba Kondoa Mjini lililoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Nchini (TGNP) pamoja na Washirika wanaotetea Haki za Wanawake Nchini akisema "wanawake wenzangu wote tujitokeze kugombea nafasi za uongozi kwa sababu yupo mwanamke Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameonyesha kuwa wanawake wanaweza,ni imani yangu wanawake wengi mtajitokeza kuwania nafasi za uongozi tukiiga mfano kwa Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye jamii imejionea kazi kubwa aliyoifanya."

"Ili usawa wa kijinsia ufikiwe ni lazima wanawake tuchukue hatua,mazingira rafiki yamewekwa hivyo kazi ni kwetu kupambana tuchukue hatua za kugombea na kuingia katika ngazi za maamuzi"ameongeza Rc Senyamule.

Pia Mhe.Senyamule ameongeza kwa kusema serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali kutekeleza mpango kazi wa Beijing kufikia usawa wa kijinsia ambapo kwa sasa wanawake wengi wameshika nafasi za uongozi Mhe.Rais akifanya teuzi kwa wanawake kwa nafasi mbalimbali zikiwemo  mawaziri,makatibu,wakuu wa mikoa na wilaya n.k

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Bi.Lilian Liundi amesema suala la usawa wa kijinsia ni suala la maendeleo akiwahamasisha wananchi kutoa maoni yao kwenye Dira ya Taifa 2050 ajili ya mwelekeo wa taifa miaka 25 ijayo kwa kuzingatia haki na usawa wa kijinsia.

 Bi.Lilian ameongeza akisema tamasha hilo ni la siku tatu kuanzia Agosti 27 hadi 29 likiongozwa na mada kuu "Dira jumuishi ya 2050 :Miaka 30 baada ya Beijing tujipange ikishirikisha Wanaharakati na Wadau zaidi ya 300 wanaotetea haki za wanawake na usawa wa kijinsia kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Bi.Gemma Akilimali amesema Tamasha la kijinsia ni moja ya majukwaa ya TGNP katika ujenzi wa nguvu ya pamoja,jukwaa likiwa ni la wazi kwa ajili ya wanawake na wadau wa haki za binadamu wakikutana kila baada ya mwaka mmoja kubadilishana mawazo.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Nchini unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024,nafasi mbalimbali zikiwaniwa zikiwemo Mwenyekiti wa Kijiji,Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji(Kundi mchanganyiko la Wanawake na Wanaume),Mwenyekiti wa Mtaa na wajumbe wa ya mtaa(Kundi mchanganyiko la wanawake na wanaume),Mwenyekiti wa Kitongoji na wajumbe wa mamlaka za miji midogo.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 12, 2025
  • RC SENYAMULE AFANYA ZIARA KONDOA DC

    May 13, 2025
  • ELIMU YA UZUIAJI UPOTEVU WA NAFAKA KUWA SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA KONDOA DC

    May 11, 2025
  • WANANCHI KIJIJI CHA ITUNDWI WAADHIMISHA KWA VITENDO SIKU YA AFYA NA LISHE

    May 07, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.