• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

VIONGOZI WA WILAYA YA KONDOA WAPIGWA MSASA KUHUSU STAKAKABADHI GHALANI.

Posted on: February 14th, 2025

Timu ya Viongozi Kondoa ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa, Wakurugenzi wake Ndg. Shabani Millao (Kondoa DC) na Ndg.Said Majaliwa(Kondoa TC) pamoja na Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri hizo wamefika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kujionea namna mfumo wa Stakabadhi Ghalani unavyofanya kazi na kujipatia mapato makubwa kwa mwaka huku jamii ikifaidika na mfumo huo.

Akifafanua namna mfumo huo unavyofanya kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Masasi Ndg.Alphaxard Etanga ameeleza kuwa mfumo huo ni mzuri na una manufaa makubwa kwa jamii na unakabiliwa na upinzani kwa Baadhi ya watu lakini inahitajika nguvu ya ziada kuufanikisha ili kukabiliana na wanaopinga mfumo huo ili mkulima apate faida  sambamba na Halmashauri kukusanyia Mapato kwa urahisi.

Kwa upande wa Afisa Ushirika Ndg.Ahmadi Selemani Issa ameeleza kuwa kwa wilaya yoyote ile inayotaka kufanikiwa katika mfumo huu ni lazima kuwepo kwa Ushirika wa mazao ya Kilimo na Masoko (AMCOS).

Ndg.Ahmadi ameendelea kwa kutoa elimu na kusema kuwa" kupitia AMCOS wakulima wanaepushwa na udanganyifu wa wafanyabiashara wanaotaka kujitajirisha kupitia mazao yao lakini pia wanaepushwa na matapeli waliokuwa wakichukua fedha zao kwani hapo awali mkulima alikuwa akilipwa fedha zake mkononi Jambo ambalo ni hatari.Mfumo huu umeboresha zaidi na kufanya malipo kwa njia za kieretroniki ili kuhakikisha kila Mdau anapata malipo yake kwa usalama na kwa haraka".

Akipokea mafunzo hayo Mhe.Fatma Nyangasa ameeleza kuwa sasa ni kwenda kutimiza yale waliojifunza kwa nguvu zote kwani uwepo wa madiwani katika mafunzo hayo ni chachu ya kufanikisha mfumo huo kwani wao pia watahusika kutoa elimu kwa wananchi wao.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya (W)Kondoa Ndg.Shabani Millao amesema kuwa amefurahishwa na mafunzo hayo huku akiahidi utekelezaji wa kina kuanzia ngazi ya kijiji mpaka wilaya kwani lengo ni kutimiza ahadi ya Rais, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumfanya mkulima kula jasho lake pasipo tabu yeyote ile.

Ameendelea kwa kusema kwamba elimu itakwenda kutolewa kwa kijiji kwa kijiji, Mtaa kwa Mtaa mpaka kitaeleweka kwani lengo ni moja kuinua uchumi wa Wananchi wa Kondoa kwenda mbele zaidi.

Sambamba na hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kondoa Bi.Hijja Suru, Katibu wa Wilaya Bwn.Hanzuruni Mtebwa pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya Bwn. Kimoro wamesema kuwa sasa kazi itakwenda kufanyika kwani kwa kufanya hivyo ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Hayo yamefanyika Februari 12, 2025 katika Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 12, 2025
  • RC SENYAMULE AFANYA ZIARA KONDOA DC

    May 13, 2025
  • ELIMU YA UZUIAJI UPOTEVU WA NAFAKA KUWA SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA KONDOA DC

    May 11, 2025
  • WANANCHI KIJIJI CHA ITUNDWI WAADHIMISHA KWA VITENDO SIKU YA AFYA NA LISHE

    May 07, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.