• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

Posted on: May 3rd, 2025

Viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wamefanya ziara ya kujifunza namna ya Utekelezaji na Uratibu wa Fedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo  katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.

Ujumbe huo umepokelewa na timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ukiwajumuisha Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Fedha, Mipango, Ukaguzi na Manunuzi wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Justice Shemakange ambaye aliwapokea katika Ofisi ya Mkurugenzi-Bukulu na kisha kuwapeleka katika Mradi wa Ujenzi wa Shule Shikizi ya Msiyauti kata ya Mnenia iliyotekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Jimbo la Kondoa na Nguvu za Wananchi.

Akiongoza Ujumbe huo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Ndg.Salhina Mwita Ameir amesema lengo la ziara hiyo ni kujengewa uelewa juu ya Usimamizi wa utekelezaji wa Fedha za Mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo VisiwaniZanzibar.

Wakiwa ziarani ujumbe huo wapata uzoefu katika suala la Uibuaji wa Miradi ya Maendeleo na Upitishaji wa Vipaumbele, Usimamizi na Uendeshaji wa kamati za fedha za kuchochea Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDCF Communities), Uzoefu katika namna ya Ufungaji wa Hesabu na Hoja za Ukaguzi, Usimamizi wa Sheria ya Fedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo na Utekelezaji wa Mwongozo wa Ununuzi kwa kutumia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo.

Akihitimisha ziara hiyo Ndg.Salhina Mwita amesema "Tunawashukuru na kuwapongeza  Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa namna mlivyojipanga katika ziara hii na sisi tumeridhika, tumeona na kujifunza mengi na mradi tuliouona unaendana na mahitaji ya jamii ambao utekelezaji wake umezingatia ufanisi mkubwa vivyo hivyo na jamii inaendelea kushajihika kuona shule inaendelea vizuri, muendeleze hizo jitihada na sisi tumejifunza tunaahidi kuyafanyia kazi. "

Akipokea shukrani hizo kaimu Mkurugenzi Ndg.Justice Shemakange,  amewapongeza kwa kuichagua kondoa kuja kujifunza kwa kubadilishana uzoefu na kuahidi  kupokea na kuufanyia Kazi ushauri uliotolewa na ugeni huo.

Ziara hiyo ni matokeo chanya ya Muungano yakichochea mahusiano yaliyotukuka kutokana na waasisi wa Muungano Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere na Hayati Sheikh Amani Abeid Karume aliyekuwa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.