• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA YAFANA KATA YA THAWI

Posted on: June 17th, 2025

Watoto wa Kata ya Thawi,Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wameungana watoto wengine wa nchi za Afrika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Hayo yamejiri mapema Juni 16,2025 katika viwanja vya Shule ya Msingi Thawi wakijumuika pamoja na Viongozi ngazi ya Halmashauri na Kata pamoja na Wazazi wa Watoto hao kusherehekea siku hiyo.

Akifungua sherehe za Maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri,Mwl.Line Chanafi ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari amesema wazazi wana jukumu la kuhakikisha mtoto analindwa dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na vipigo, kuchomwa moto, ubakaji, ulawiti na kutogwa na vitu vyenye ncha kali vikitokomezwa vitendo hivi kwa kuwashirikisha watoto katika kutoa taarifa za viashiria vya ukatili wanaofanyiwa wakiwa shuleni, nyumbani , na maeneo mengine.

"Sisi kama wazazi tujitahidi kuwatimizia watoto wetu mahitaji yao ya msingi bila kubaguliwa kwa jinsi zao  yakijumuisha chakula chenye lishe,huduma za Afya,Elimu,Mavazi na Malazi.Mtoto aliyepatiwa mahitaji yake ya msingi sio rahisi kushawishika kujiingiza kwenye tabia hatarishi." Ameongeza Mwl.Chanafi.

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri Bi.Rahiya Nasser amesema lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuwaweka pamoja,wakikumbushana thamani,utu na umuhimu wa mtoto katika ngazi ya familia, jamii,na taifa kwa ujumla likienda sambamba na Kaulimbiu isemayo "Haki za Mtoto : Tulipotoka, Tulipo na Tuendako".

Naye Diwani mwenyeji wa kata ya Thawi Mhe.Juma Hapi ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi kwa kuichagua kata hiyo kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ngazi ya Halmashauri,akiwaasa wananchi na wazazi kuyafanyia kazi maagizo ya Mgeni rasmi dhidi ya Maadhimisho hayo.

Kila mwaka tarehe Juni 16,Serikali ya Tanzania huungana na nchi zingine  za Afrika kusherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo kwa ngazi ya Halmashauri yamefanyika katika Shule ya Msingi Thawi.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • ELIMU YA BAJETI YA MLENGO WA KIJINSIA KUINUFAISHA KONDOA

    June 26, 2025
  • STAKABADHI GHALANI MUAROBAINI ENDELEVU KWA WAKULIMA WILAYA YA KONDOA

    June 25, 2025
  • WALIMU NA MAAFISA ELIMU KATA KONDOA DC WAJENGEWA UWEZO WA USIMAMIZI UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI

    June 21, 2025
  • WARAGHIBISHI MASUALA YA KIJINSIA WILAYA YA KONDOA WAJENGEWA UWEZO

    June 21, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.