• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

RAS DODOMA ATETA NA WATUMISHI KONDOA DC

Posted on: March 28th, 2024

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ndg.Kaspa Kaspa Mmuya amefanya ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, hii inafuatia uteuzi wa Ndg.Kaspa Kaspa Mmuya kuteuliwa na Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni.

Ndg. Mmuya amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Watumishi wa Halmashauri katika Ukumbi wa Mikutano ,Jengo la Utawala wakiwemo Wakuu wa Divisheni ,Vitengo,Watendaji wa kata na Vijiji pamoja na Watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri.

Ndg.Mmuya ametumia nafasi hiyo kuwapongeza watumishi kwa kazi kubwa wanayoifanya katika utatuzi wa changamoto zinazowakumba wananchi wakiongozwa na kauli mbiu isemayo’’ KERO YAKO, WAJIBU WANGU’’.

Ndg. Mmuya katika kikao  hicho na watumishi amegusia mambo mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa nguvu ya ukusanyaji wa mapato ya ndani,uwajibikaji wa kimkakati kwa kuonyesha mfano kwa kuhusika katika shughuli za maendeleo,usimamizi mzuri wa shughuli za maendeleo,uhimizaji wa kilimo cha zao la kimkakati la Alizeti,Utendaji haki ,Ufaulu kwa Wanafunzi kupitia ufatiliaji makini kwa mahudhurio ya wanafunzi kwa kuzingatia ushirikiano baina ya wanafunzi ,walimu na wazazi ,dhana ya mahusiano baina ya watumishi iwe nguzo kwa kuimarisha nguvu kazi.

Akifafanua majukumu hayo Ndg.Mmuya alisisitiza ufanyaji wa vikao vya kisheria ambapo kero mbalimbali kutoka chini zinakusanywa na kufikishwa kunakohusika.

Sambamba na hayo Ndg.Mmuya alipata wasaa wa kukagua na kupokea taarifa za miradi ya maendeleo ikiwemo Jengo la Utawala,Nyumba ya Mkurugenzi pamoja na Majengo ya hospitali ya Wilaya akiambatana na timu ya wataalam kutoka Mkoani na Wilayani.

Kwa niaba ya watumishi wa halmashauri Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Shaban Millao ametumia nafasi hiyo kumpongeza katibu tawala kwa kuteliwa na Mh.Rais na kuhaidi kuyafanyia kazi maelekezo aliyoyatoa.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.