• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MWENYEKITI WA HALMASHAURI KONDOA DC AIPONGEZA CMCR -DODOMA

Posted on: January 26th, 2025

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mhe.Abdalah Maguo ameshukuru na kupongeza Shirika lisilo la kiserikali CMCR-Dodoma kwa kuwezesha wahudumu wa afya wa Halmashauri na wahudumu afya ngazi ya jamii.

Hayo ameyasema katika kikao cha Tathmini ya pamoja dhidi ya Ugonjwa wa Kifua kikuu na UKIMWI katika hafla fupi ya ukomo wa mradi unaofadhiliwa na shirika hilo, akiahidi msimamo wa Halmashauri katika usimamiaji wa vifaa wezeshi ili kuendelea kufanya kazi na kuvifanyia matengenezo pale inapohitajika.

"Kama halmashauri tutahakikisha yale yote ambayo yalianzishwa na CMCR kuisaidia Halmashauri yetu yanakua endelevu na nawaelekeza wataalam wetu ngazi ya Halmashauri na wahudumu ngazi ya jamii kuendelea kuwabaini waathirika wa magonjwa haya, kwa kutoa elimu ya kutosha" amesisisitiza Mhe.Maguo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Ruta Chunzibwa amesema halmashauri ya wilaya ya Kondoa ni mojawapo ya halmashauri za Mkoa wa Dodoma zilizopata nyenzo za kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Kifua kikuu kwa Imani kwamba washiriki wa kikao hicho wataenda kufanya vizuri ili kupunguza maambukizi ya magonjwa hayo.

Naye Meneja Mradi Dkt.Hamoud Ndenge katika taarifa yake amesema, mradi ulijikita katika kupunguza maambukizi ya VVU na Kifua kikuu kwa kuwajengea uwezo watumishi halmashauri, utoaji vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya Halmashauri, kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ngazi ya jamii na kuwapa vitendea kazi wahudumu hao.

Kikao hicho kimefanyika  Ukumbi wa Mikutano wa Kanisa Katoliki Kondoa Mjini na kuwakutanisha Wawakilishi kutoka Wizara ya Afya, TAMISEMI, Kamati ya kusimamia huduma za afya mkoa (RHMT) na Halmashauri (CHMT) pamoja na Waganga wafawidhi kutoka vituo vyote 26 vya kutolea huduma za afya halmashauri ambavyo mradi huu umetekelezwa.

Katika kipindi chote cha mradi, Halmashauri imenufaika kwa kukarabatiwa kwa vituo 8 vya kutolea dawa za kifua kikuu (Dot Center), Ununuzi wa Samani, Usimikaji wa Mifumo ya Sola katika vituo  6 vya kutolea huduma.

Miongoni mwa vituo vya kutolea huduma vilivyonufaika ni pamoja na Kituo cha Afya cha Bereko,Thawi,Kalamba,Mnenia, Pahi, Busi, Itololo, Mauno pamoja na baadhi ya  Zahanati.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 12, 2025
  • RC SENYAMULE AFANYA ZIARA KONDOA DC

    May 13, 2025
  • ELIMU YA UZUIAJI UPOTEVU WA NAFAKA KUWA SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA KONDOA DC

    May 11, 2025
  • WANANCHI KIJIJI CHA ITUNDWI WAADHIMISHA KWA VITENDO SIKU YA AFYA NA LISHE

    May 07, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.