• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKURUGENZI MILLAO AKABIDHI VITENDEA KAZI KWA MAAFISA UGANI NA WATENDAJI KONDOA DC

Posted on: September 6th, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao amekabidhi vitendea Kazi kwa Maafisa Ugani na Watendeji vikiwemo Pikipiki,Vishikwambi na Sare za Kilimo (Overall)  ili kuongeza ufanisi kwa wataalam hao kwenye majukumu yao.

Akikabidhi vitendea kazi hivyo Ndg.Millao amewataka wataalam hao kuvitumia vitendea kazi hivyo ipasavyo ili kusikiliza na  kutatua kero za wananchi (Watendeji waliokabidhiwa Pikipiki)na Matumizi lengwa ya Vishikwambi kuwasaidia wakulima kulima Kilimo chenye Tija (Maafisa Ugani waliokabidhiwa Vishikwambi na Sare).

"Serikali ina malengo makubwa kwa Mkulima kwa kuhakikisha analima kwa tija ili kuchangia Maendeleo yake binafsi na Maendeleo ya nchi kwa ujumla. "Mh.Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan ameweka matumaini makubwa kwenye Kilimo kwa kuongeza bajeti ya Kilimo kutoka Bilion 200-300 kwa mwaka kabla ya mwaka 2021 hadi kufikia zaidi ya Tshs Trilioni 1.2 ikiwa ni mara nne zaidi ili kumsaidia mkulima kulima kilimo chenye tija kitakachochangia pato la Taifa."amesema Ndg.Millao.

Ndg.Millao amesema Injini ya Halmashauri ni Kilimo, kupitia Matumizi ya Vishikwambi hivyo usajili wa wakulima ufanyike ili kusaidia kupata takwimu sahihi, kushirikiana vyema na viongozi wa serikali kumsaidia ili mkulima na wananchi wa vijiji husika wakanufaike na Kilimo chako hasa kwenye skimu za umwagiliaji.

Sambamba na hayo Ndg.Millao amewaagiza Maafisa Ugani kusimamia vyema mfumo wa Stakabadhi ghalani kupitia mazao ya Mbaazi na Dengu, kwa kutoa Elimu ya kutosha kwa wakulima juu ya umuhimu wa mfumo huo wenye lengo la kumsaidia mkulima kuuza mazao yake kwa bei nzuri pia amewasihi wakulima wenyewe ndiyo wajitahidi kupeleka mazao yao na sio kuwauzia madalali.

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg.Juvenal Munishi amesema serikali kupitia wizara ya Kilimo imekabidhi Vishikwambi 23 na Sare 23 Kati ya 59 vinavyotakiwa, ikiwa ni awamu ya Kwanza kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya Kondoa. Vishikwambi hivyo vitakavyotumika kupima ukubwa wa maeneo ya Kilimo, kuchukua Sampuli za Udongo n.k ili kumsaidia mkulima kufuata Kanuni bora za uwekezaji kwenye Kilimo.

Pia kwa upande wa Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali watu Ndg.Peter Ngomuo amesema Serikali imekabidhi Pikipiki 3 kwa Watendaji wa 3 wa Kata Kata za Mnenia,Kalamba na Kisese zitakazosadia Watendeji wa Kata husika kuwafikia wananchi kwa urahisi ili kusikiliza na kutatua kero zao. Idadi hii imefanya jumla ya Pikipiki tisa kwani awali Serikali ilishatoa Pikipiki sita. Pia Halmashauri imepanga kununua Pikipiki tano kwa bajeti ya mwaka huu wa fedha kutoka katika fedha za ufuatiliaji.

Pia katika hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi hivyo watumishi wapya walioajiriwa Mwezi Julai mwaka huu 2024 katika Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wapatao 16 walitambulishwa ambao watumishi 5 ni kada ya Mifugo na watumishi 11 ni kada ya kilimo.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2025 June 06, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 12, 2025
  • RC SENYAMULE AFANYA ZIARA KONDOA DC

    May 13, 2025
  • ELIMU YA UZUIAJI UPOTEVU WA NAFAKA KUWA SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA KONDOA DC

    May 11, 2025
  • WANANCHI KIJIJI CHA ITUNDWI WAADHIMISHA KWA VITENDO SIKU YA AFYA NA LISHE

    May 07, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.