• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

*MAMLAKA YA UDHIBITI WA MBOLEA (TFRA) YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA UGANI*

Posted on: March 3rd, 2025

Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea (TFRA)  imeendesha mafunzo ya kuwawezesha Maafisa Ugani kutoka Halmashauri ya Kondoa  na Kondoa Mji  namna ya kutumia Vishkwambi  katika kuendesha shughuli zao.

Mafunzo haya ya siku moja yamefanyika tarehe 28/02/2025, yakilenga kuwaongezea ujuzi maafisa Ugani hao, kuwajengea uwezo wa kuwasajili wakulima katika mfumo, kuhuisha taarifa za wakulima pamoja na kutoa taarifa sahihi za wakulima kupitia Vishkwambi hivyo.

Msingi wa mafunzo haya ni kurahisisha  huduma zote zinazotolewa na Wizara ya Kilimo kwenda kwa wakulima ikiwemo uuzwaji wa Pembejeo kwa wale wakulima waliokwisha sajiliwa.

Mkufunzi wa mafunzo hayo Ndg. Allan Mariki ambaye pia ni Meneja wa kanda ya kati kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Tanzania, ameeleza umuhimu wa kutumia Vishkwambi hivyo kwa maafisa Ugani hao. " Moja ya lengo la Kishkwambi hiki, ni kumuwezesha Afisa Ugani kumsajili mkulima kwenye ngazi ya Kata, hivyo ni mategemeo yetu kwamba idadi ya wakulima itaongezeka ndani ya muda mfupi".

 Ndg. Rabeca Amos Robson, Afisa Ugani kutoka Halmashauri ya Kondoa DC, kijiji cha Sakami, ameelezea namna ambavyo wameyapokea mafunzo hayo na namna ambavyo watakwenda kuyafanyia kazi " Tumepokea vizuri mafunzo na yataturahisishia kazi kwa sababu inatupa nafasi ya sisi kuwasajili papo kwa papo"

Akihitimisha mafunzo hayo Meneja wa Kanda ya Kati wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Ndg. Allan Mariki, alisema zoezi hili ni endelevu mara baada ya Maafisa Ugani hao kupokea Vishkwambi hivyo zoezi litakua endelevu kutokana na mbinu mbalimbali za Kiteknolojia zitakavyokua zinakuja.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.