• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

LISHE BORA KWA WATOTO NA KUTOWAFICHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM MAJUMBANI VYAHIMIZWA -KATA YA HONDOMAIRO

Posted on: September 6th, 2024

Wananchi wa Kata ya Hondomairo kupitia siku maalum ya kuongea na wazazi na wanafunzi wanaohitimu Elimu ya Msingi shule za Dorasi, Hondomairo, Mwembeni, Isari, Swagaswaga na Misreyi wamehimizwa kuzingatia lishe kwa watoto pamoja kutokuwaficha watoto wenye mahitaji maalum majumbani mwao.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa siku hiyo maalum ya wanafunzi wa Shule za Msingi za kata ya Hondomairo akiwahimiza wazazi kuchangia huduma ya Chakula kwa wanafunzi wa madarasa yote badala ya wanafunzi wa madarasa ya mitihani pekee. Amewaasa Wazazi kuacha tabia ya kuwaficha majumbani watoto wenye mahitaji maalum akisema ni kuwanyima haki yao ya msingi kama watoto wengine pamoja na malezi Bora kwa watoto.

"Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi TSh.Bil 9 katika Elimu kwa halmashauri yetu zikitumika kuboresha miundombinu ya Elimu, matarajio ni kuona watoto wanapelekwa shule na wanafanya vizuri" amesema "kufanya hivyo ni kumuunga Mkono Mhe. Rais" amemalizia Ndg. Millao.

Kwa upande wa Wahitimu, Ndg. Millao amewataka kujiandaa vyema dhidi ya Mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi utakaofanyika tarehe 11 hadi 12 mwezi Septemba 2024 wakisoma kwa bidii na kuahidi kutoa zawadi kwa wanafunzi watakaopata alama A katika masomo yote. Pia amewaasa kuwa na subira na tamaa zisizokuwa na muhimu kwani hiyo ni hatua moja bado wanaingia katika hatua ambayo ni ngumu kwao na kwamba wanahitaji kukataa vishawishi vyovyote vitakavyowafanya kukatisha ndoto zao.

Sambamba na suala la elimu, Ndg.Millao amewagusia wananchi wa kata hiyo juu ya upandaji na utunzaji wa miti 20  kwa kila kaya ili kulinda mazingira yetu, amewaomba pia kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, kuchagua na/kuchaguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024. Jambo lingine ambalo Ndugu Millao amelisisitiza ni suala la usalama wa jamii yetu kwa kuwataka kuwatambua wageni wanaofika kwenye maeneo yao kutoa taarifa ofisi za vitongoji na kijiji ikiwa ni pamoja na kuwaandikisha katika daftari maalumu la wageni. pamoja na kuwapongeza Walimu pia amewaasa wakulima kutumia Mfumo wa Stakabadhi ghalani ili kuongeza tija ya mazao ya kimkakati Ikiwemo Mbaazi na Dengu. Amewaeleza faida ya kutumia mfumo huo kwa wakulima wenyewe na si madalali.

Mkurugenzi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo alianza kwa kusikiliza na kutatua kero za wazee wa kata hiyo.

Shule za Msingi kata ya Hondomairo zinasifika kwa kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa, katika Mtihani wa Pre-Necta mwaka 2024 shule ya msingi Misrey na Swagaswaga zilipata ufaulu wa 100% na 93%

Pia katika mwaka wa masomo 2024 jumla ya Wahitimu 272(Wasichana 150 na Wavulana122) kutoka shule hizo wanatarajiwa kufanya Mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.