• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

KONDOA DC YANUNUA MASHINE ZA VIRUTUBISHI KUKUZA HALI YA LISHE KWA WANAFUNZI NA JAMII

Posted on: January 6th, 2025

Kamati ya lishe Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imepokea taarifa ya ununuzi wa Mashine maalum za Virutubishi zitakazosaidia kukuza hali ya Lishe Bora kwa Wanafunzi na Jamii.

Akiwasilisha taarifa yake kwa kamati hiyo iliyoketi kwa ajili ya Kikao cha Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Lishe mwaka wa fedha 2025/2026 Afisa Lishe Ndg.Khamis Faki amesema halmashauri imenunua na kufunga mashine mbili za virutubishi kutoka Kampuni ya SANKU zenye Thamani ya Tsh Mil 3 na Laki 2 kwa kata ya Soera na Bereko kwa ajili ya wanafunzi na jamii ambazo zimefungwa katika viwanda vidogo vidogo vya kusaga unga wa mahindi.

Ndg.Faki amesema matarajio ya halmashauri ni kuongeza mashine 6 kati ya 8 zitakazofungwa kata za Kikore, Kisese,Pahi,Bumbuta,Busi na Thawi ambazo matarajio yake ni kuzinufaisha Shule za Msingi na Sekondari pamoja na jamii kwa ujumla juu ya kuongeza thamani ya chakula chenye mchanganyiko wa virutubishi lengo likiwa ni kukuza hali ya lishe bora kwa jamii.

Sambamba na ununuzi wa mashine hizo halmashauri imefanikiwa kuwaibua na kuwatibu watoto wenye utapiamlo mkali kwa 100%,Utekelezaji wa kampeni ya Utoaji wa Matone ya Vitamin A na Dawa za Minyoo ambapo watoto chini ya miaka 5 wamefikiwa  kwa 118% pamoja na uongezekaji wa idadi ya wanafunzi wanaopata chakula shuleni kutoka 51% mwaka 2023/2024 hadi 75% kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba 2024.

Pia kamati imepokea taarifa ya fedha iliyotengwa kwa kipindi cha mwaka 2024/2025 ,Tsh 108,593,383.75/=na kilichotumika ni Tsh. 27,723,000 sawa na asilimia 25.5 ikikubaliana kujikita katika vipaumbele mbalimbali ikiwemo kila Divisheni kutoa fedha za lishe kama zilivyopangwa,kuongeza Idadi ya wanafunzi wanaopata chakula shuleni,kuongeza idadi ya shule na kaya  zenye bustani za mbogamboga na miti ya matunda pamoja na Ufugaji wa samaki na Wanyama kwa ajili ya lishe.

Kikao hicho kimewakutanisha wajumbe kutoka Ofisi ya Mkurugenzi ikizijumuisha Divisheni ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii, Elimu Awali na Msingi,Elimu Sekondari, Kilimo,Mifugo na Uvuvi pamoja na Divisheni ya Maendeleo ya Jamii.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.