• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo ,Mifugo na Uvuvi
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijiji na Mijini
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Bee
      • Sheria
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DED MILLAO AWAONGOZA WANANCHI ZOEZI LA USAFI SHULE MPYA SEKONDARI YA MNENIA

Posted on: January 23rd, 2025

Mapema Januari 22, 2025, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao, timu ya Wataalam kutoka Halmashauri pamoja na Wananchi wa kijiji cha Mnenia Kata ya Mnenia wamejumuika pamoja katika usafi wa mazingira ya Shule Mpya ya Sekondari ya Mnenia.

Katika zoezi hilo Ndg.Millao amewapongeza wananchi hao kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha kwa kipindi chote cha ujenzi wa Sekondari hiyo kwakuonyesha juhudi binafsi za kujenga Darasa kwa nguvu za wananchi.

"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutambua jitihada zenu za uhitaji wa shule ya Sekondari ilitenga fedha zaidi ya Tzs Mil 544 ambazo zimetumika kujenga miondombinu ya kisasa kwa watoto wetu kusomea, tuna kila sababu za kuishukuru serikali yetu, jitihada za Mhe Mbunge wetu Dkt.Ashatu Kijaji pamoja na Diwani mwenyeji Mhe.Abdalah Maguo zimesaidia shule hii kufikia hapa". Amesema Ndg.Millao

Ndg.Millao asema lengo la Serikali ni kuhakikisha wanafunzi wanapata Elimu bora katika mazingira rafiki ikipunguza umbali mrefu zaidi ya KM 7 kufuata elimu katika Shule ya Sekondari IMBAFI, na kuwataka  wazazi kufuatilia maendeleo ya wanafunzi hao.

Kwa upande wake Mhandisi wa Halmashauri Eng.John Chizima amesema shule hiyo imejengwa kwa fedha za Serikali kupitia mfumo wa "Force Account" ambao huwanufaisha wananchi wa mradi ulipo, kupongeza hali ya usalama wa vifaa vilivyotumika kipindi chote cha ujenzi pasipo uharibifu wowote kufanywa na wananchi hao na baadhi yao kuwa miongoni mwa mafundi wanaojenga majengo hayo.

Nao baadhi ya Wananchi waliojitokeza shuleni hapo wamemshukuru Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za Ujenzi wa Shule hiyo Mpya ambayo itarahisha kupunguza umbali mrefu kwa wanafunzi.

Shule Mpya ya Sekondari Mnenia  inatarajiwa kupokea Jumla ya Wanafunzi 125 wa kidato cha kwanza mwaka huu 2025 pamoja na wanafunzi wasiopungua 60 wa kidato cha pili watahamishwa kutoka shule mama Sekondari ya IMBAFI.

Katika kuzingatia umuhimu wa lishe na utunzaji wa mazingira, jumla ya Miti 550 ikijumuisha Miti ya matunda 250 na Miti zaidi ya 300 ya kivuli imepandwa kuzunguka mazingira ya shule.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 06, 2025
  • JEDWALI LA MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 24, 2024
  • UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA October 15, 2024
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI KONDOA DC WAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

    May 04, 2025
  • VIONGOZI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO-KONDOA DC

    May 03, 2025
  • MAJIBU YA HOJA ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SASA KUFANYIKA KIDIGITALI

    April 16, 2025
  • MKURUGENZI MILLAO AONGOZA BONANZA LA MNENIA KUELEKEA MWENGE WA UHURU 2025

    April 16, 2025
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.