• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kondoa District Council
Kondoa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
      • Background
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Administration and Human Resources
      • Fedha na Biashara
      • Planning ,Monitoring and Statistics
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Msingi
      • Elimu sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Agriculture ,Irrigation and Cooperation
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Procurement
      • Election
      • Bee
      • Legal
      • Information and Communication Technologies (ICT)
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Finance and Planning
      • Mipango na Mazingira
      • Economy ,Health and Education
      • AIDS
      • Maadili
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Jinsi ya Kulipia Leseni za biashara

kupata leseni y biashara hakikisha una TIN namba toka TRA

 UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA

Leseni zote za Biashara hutolewa chini ya sheria ya Biashara Na.25 ya Mwaka 1972 na Marekebisho yake yaliyofanyika june 2014 pamoja na marekebisho katika sheria ya Fedha Na.2 ya Mwaka 2014 na Na.16 ya Mwaka 2015. Mwombaji wa leseni ya biashara  anapaswa ajaze fomu ya maombi ya leseni TFN211 (Business application form).

Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane(18) Mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara kisheria.

Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinacho mruhusu kufanya biashara nchini kutoka idara ya uhamiaji.

LESENI ZA BIASHARA ZIMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI MAWILI:

KUNDI A;Leseni hizi hotelewa na Wizara ya Viwanda ,Bishara na Uwekezaji.(Fomu ya maombi iwasilishwe na Halmashauri kabla ya kupelekwa Wizarani)

Mfano;

  • Uagizaji bidhaa toka nje(import licence)
  • Kusafirisha bidhaa nje (Export licence)
  • Hotel za kitalii (Tourist Hotel& Lodging)
  • Wakala wa kupokea na kusafirisha mizigo (Clearing and Fowarding/Freight Forwarders) n.k

KUNDI B:Hizi hutolewa na Halmashauri za Wilaya,Manispaa,Miji na Majiji husika.

Mfano:

  • Wakala wa Bima (Insurance Agent)
  • Vipuri (Spare parts,Mshine tools)
  • Maduka ya dawa za Binadamu/Mifugo
  • Viwanda Vidogo (Small Scale Manufacturely and Selling)
  • Uuzaji Bidhaa Jumla na Rejareja (Wholesale and Retail trade) n.k

UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA

Kila Mfanyabiashara anatakiwa afike ofisi ya Biashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa ajili ya kuchukua fomu na kujaza kama utakavyoelekezwa .Baadhi ya nyaraka zinazohitajika kama kiambatanisho na masharti katika fomu ya maombi (TFN221) ni ;

  • Mfanyabiashara anapaswa awe na hati ya usajili iwapo anatumia jina la biashara      ( Certificate of Registration or Incorporate).
  • Kama ni Kampuni mwombaji awe na memorandum and Article of Association ambazo zinaonyesha kuwa kampuni imeruhusiwa kufanya biashara anayoiomba.
  • Mwombaji awe na umri wa miaka 18 au zaidi
  • Awe na mahali/Eneo linalokubalika kwa aina ya biashara anayoiomba  na isiwe vidanda vilivyopo kando kando ya barabara.
  • Awe na TIN certificate.
  • Awe na hati ya kuthibitisha uraia wake kama,Nakala ya Hati ya Kusafirisha”passport”ya Tanzania,cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo(Affidavit) au Kitambulisho cha Mpiga kura.Kama ni mgeni awe na hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Resident Permit Class “A”.)
  • Masharti mengine ya kupata leseni hutegemea aina ya biashara mtu anayetaka kuanzisha  e.g. Mgahawa,Dawa za Binadamu na Mifugo,Vyakula,Nyama na Samaki inabidi afuate taratibu zote za afya na kupima wafanyakazi wake
  • Hati ya Utaalam (Professional Certificates) kwa biashara zote za kitaalam
  • Maombi mapya yatapitia ngazi za Serikali ya Mtaa/kijiji ,Afya na Kisha ofisi ya biashara kwa ajili ya utoaji wa leseni.

MALIPO:Kutokana na marekebisho ya sheria ya fedha Na 2 ya mwaka 2014 ada za leseni hulipwa kulingana na aina ya biashara kama ilivyoanishwa katika jedwali la viwango vya ada kwa mwaka

MUDA WA LESENI: Umri wa leseni ni miezi 12 toka siku ya kutolewa.

 

MASHARTI YA UTUMIAJI WA LESENI

1.Mwenye leseni hataweka masharti yeyote kwa mnunuzi

2. Mwenye leseni atatoa risiti kwa mauzo yote.

3.Mwenye leseni atafuata sheria ya leseni ya biashara No. 25 ya 1972

4.Mwenye leseni hatatoa huduma/bidhaa ambazo hazizingatii viwango vya ubora,uliowekwa na Vyombo vinavyotumika kisheria

5.Mwenye leseni anaweza kunyang’anywa wakati wowote ikiwa inaonekana aliipata kwa njia ya udanganyifu au amekiuka masharti ya leseni.

MAKOSA

   1.Kuendesha biashara bila leseni

   2.Kuendesha biashara eneo tofauti na linaloonyeshwa kwenye Leseni.

  3.Kutumia leseni moja kufanya biashara zaidi ya moja au maeneo mawili au zaidi

  4.Kushindwa kuonyesha leseni ya biashara inapotakiwa kufanya hivyo na Afisa aliyedhinishwa na Serikali.

  5.Kutokuweka leseni ya biashara mahali ambapo inaonekana kwa urahisi (Kuficha leseni).

  6.Kutoa maelezo ya uongo ili kupata leseni au kukwepa kulipa ada /kodi inayostahili

  7.Kumzuia Afisa wa Serikali aliyepewa mamlaka ya kukagua kufanya kazi yake.

ADHABU;  (i). Mtu yeyote anayetenda mojawapo ya makosa hapo juu adhabu yake ni faini isiyopungua Tsh 50,000/= na isiyozidi Tsh 100,000/= au kifungo kisichozidi miaka miwili(2) au faini na kifungo kwa pamoja.

                  (ii). Mtu yeyote atakayechelewa kuhuisha leseni yake baada ya siku 21 baada ya     muda wa leseni kuisha atalipia asilimia 25 ya ada iliyotakiwa kulipia na itaongezeka asilimia 2 kila mwezi kadri mfanyabiashara anavyochelewa kuhuisha leseni ya biashara

NB.Wafanyabiashara wote wanaaswa kufuata na kutekeleza sheria bila shuruti,kwani kutofanya hivyo kunawaingiza gharama zisizo za lazima kama faini na kupoteza muda hasa pale wanapokutwa na makosa

Pakua Fomu ya Maombi ya Leseni Hapa Chini

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI March 02, 2023
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2022 January 29, 2023
  • Uandikishaji wa watoto wa darasa la awali na darasa la kwanza. December 14, 2022
  • MATOKEO YA USAHILI WA MAHOJIANO YA ANA KWA ANA RMA November 22, 2022
  • Fungua zaidi

Habari Mpya

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022

    January 29, 2023
  • WALIMU 896 WAGAWIWA VISHIKWAMBI WILAYANI KONDOA

    January 16, 2023
  • BARAZA LA MITIHANI (NECTA) LA TANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA UPIMAJI KIDATO CHA PILI

    January 04, 2023
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VETA

    December 23, 2022
  • Fungua zaidi

Video

"Kipaumbele changu Kondoa ni Elimu"-Dkt. Ashatu Kijaji(MB)
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Ruhusa
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi portal
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Chuo cha mipango Dodoma
  • Chuo kikuu Mzumbe
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ajira
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo Ramani

Wasiliana Nasi

    KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE

    Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa

    Simu : 0262360313

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.