Zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura linatarajiwa kuanza kufanyika kuanzia tarehe 8/10/2019 katika vijiji na vitongoji vyote katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa,ambapo linatarajiwa kudumu kwa muda wa siku saba(07).
Katika kuhakikisha hilo linafanyika ka mujibu wa sheria za uchaguzi wa serikali za mitaa,washiriki wote katika zoezi hilo wamekula kiapo ili kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa weledi na kwa mujibu wa sheria.
Hakimu wa mahakama ya mwanzo Mhe. Elizabeth Justine Kaiza amewaapisha washiriki wote ambao kisheria wanatambulika kwa makundi ya Afisa Mwandikishaji Msaidizi ngazi ya Kitongoji,Afisa Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata(ARO),Afisa Msimamizi Msaidizi ngazi ya Wilaya.
Kabla ya kuapisha mkundi hayo,Mhe. Hakimu aliwasisitiza Washiriki wote kuwa makini na zoezi kwani kwa kiapo wanachoapa/tamka watawajibika kwa uzembe na makosa yoyote yatakayojitokeza kipindi chote cha zoezi ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria(Mahakama)
Matukio picha wakati wa kul a kikao cha kula kiapo
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,KILIMANI STREET
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.