Shirika lisilo la kiserikali la Graling Future Foundation (GFF) chini ya uongozi wa Mkurugenzi wake mwana dada mahili Bi,Aisha Msantu tarehe ya leo amekabidhi jumla ya madawati hamsini(50) ikiwa ni ahadi yao waliokua wameitoa mbele ya Mheshimiwa Mbunge Dr.Ashatu Kijaji ,akiongea katika makabidhiano ya madawati hayo Aisha alisema wao kama taasisi wameamua kufanya hivyo hii nikutokana na mambo ambayo mheshimiwa mbunge anayafanya katika kuiletea kondoa maendeleo.Akitaja miongoni mwa vitu vilivyomvutia nipamoja na ujenzi wa daraja la masange,kisese na daraja la baura lililoko kata ya kalamba pia ujenzi wa vituo vitano vya afya bila kusahau uchimbaji wa visima maeneo mbalimbali ndani ya kondoa.
Hakuishia hapo, Bi Aisha alisema sekondari ya Kinyasi ilikua na upungufu wa madawati 94 awamu ya kwanza ametoa 50 lakini hajachoka kasema pia anaomba wamwachie amalizie na hayo 44 yaliobakia ilikukata kiu ya wanafunzi wa kinyasi pia wananchi wa kata ya kinyasi,anasena Aisha na hapa namnukuu nimeamua kufanya haya hii nikutokana na adha wanayokutana nayo wanafunzi wa shule hii pia ukarimu walionao wananchi wa kijiji hiki na kata nzima jinsi walivyotupokea na jinsi wanaavyojitoa katika kuhakikisha wanaimarisha na kuendeleza taaluma katika shule hii. Ninachowaomba watoto someni kwa bidii sana katika kujiletea maendeleo pia nawaza kuongeza matundu ya vyoo kama wananchi watajitoa katika kuchangia nugvu kazi.katika zoezi hilo pia liliambatana na kukabidhi mabox kumi ya taulo za kike nia na madhumuni nikupunguza utoro wa mara kwa mara kwa watoto wa kike hasa wanapokua katika hedhi lengo nikumsitiri mtoto wa kike ili aweze kutimiza ndoto zake za maisha.
Wakati hayo yakifanyika shughuli nzima ilipambwa na kunogeshwa na wanafunzi wa kidato cha tatu ambao waliimba shairi lao ambalo limetaja matatizo na changamoto zinazo wakabili wao kama wanafunzi pia walimu wao mambo hayo ni ukosefu wa nyumba za walimu ,upungufu wa madarasa,matundu ya vyoo,hostel,maji ,umeme pia maabara.Wanafunzi hao walitoa kilio hicho mbele ya ya mh Mbunge, pia kwa wadau mbalimbali ilikuboresha mazingira yao ya kujifunzia.Kero hizo ambazo zilitajwa na wanafunzi hao pia zilijitokeza kwenye risala iliyosomwa mbele ya mbunge na mkuu wa shule hiyo Bi Elizabeth Sanga.
Akipokea madawati hayo 50 na mabox 10 ya taulo za kike mh,Ashatu alisema yeye kazi yake nikuhakikisha anatimiza kila ambacho alikiahidi kwa wanakondoa kua kipaumbele chake ni Elimu na atahakikisha hilo linatimia pia alisema .Pia katika kujibu kero za wana jamii ya wanakinyasi mh Ashatu alisema kero ya maji katika shule hii anaifanyia kazi na akasema hapa namnukuu"kwa upande wa maji tumechimba kisima kisese sekondari ,itafuata Bukulu sekondari ,kalamba shule ya msingi nakisima cha nne kitachimbwa kinyasi sekondari na hili litafanyika hivi punde".Kwa upande wa suala la umeme napambana kuhakikisha taasisi zote zinapatiwa ikiwa ni pamoja na shule za sekondari zote ,shule za msingi ,vtuo vya afya na zahanati.
Mheshimiwa mbunge alikabidhi madawati hayo kwa mkurugenzi wa halmashauri ndg Mustapha Semwaiko ambae katika hafla hiyo aliambatana timu nzima ya wakuu wa idara ilikuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na kuona juhudi za mbunge katika kuleta maendeleo nakuahidi kuyatunza madawati hayo ili yatumike na kwa vizazi vijavyo.
Pia makamu mwenyekiti wa halmashauri mh sulu akiwa na mwenyekiti wa ccm wilaya mh Gora walisifu juhudi hizo na kupongeza mshikamano unaooneshwa na viongozi wote na wataalam wa kisekta kwa ujumla. Hakika zoezi limeenda vizuri na kufana sana hakika mama unapiga kazi hayo ni maneno yaliosikika toka kwa umati uliokusanyika eneo la kinyasi sekondari.Katika picha ni mkurugenzi wa GFF Bi Aisha akicheza na mh mbunge huku wakishangiliwa na wanakinnyasi.
.Habari na mwandishi wetu .chanzo cha habari ni www.kondoadc.go.tz.
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,KILIMANI STREET
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.