Naibu waziri wa maliasili na utalii Mhe, Japhet Hasunga hayupo pichani amezuru kondoa kwa ziara maalum ya kikazi leo tarehe 14/04/2018,Katika ziara hii ametembelea pori la akiba mkungunero ambalo ni miongoni mwa mapori tengefu 26 yaliopandishwa hadhi na kua hifadhi mwaka 1996.Pamoja na kufika katika hifadhi hii pia amekutana na wafugaji ambao mifugo yao inashikiliwa na askari wa wanyama pori kwa kosa la kulisha mifugo yao ndani ya hifadhi.Miongoni mwa wafugaji walalamikaji ni pamoja na Yohana Bilo ambae takribani ng'ombe wake 299 kati ya 1298 wanaoshikiliwa ndani ya hifadhi kwa kosa la kulisha mifugo ndani ya hifadhi kinyume cha sheria.
Baada ya kuulizwa na waziri endapo anajua kua nikosa kulisha mifugo nakuishi ndani ya hifadhi alikiri kua ni kosa pia anatambua uwepo wa hifadhi hiyo na kwamba siyo mgeni wa eneo hilo maana yeye ni mkazi wa kijiji cha Ikengwa jirani na hifadhi baada ya kupewa maelezo ya kina toka askari wa wanyama pori na pia kwa wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi , mhe, waziri alisisitika kua elimu zaidi inapaswa kutolewa kwa wananchi wanaopakana na hifadhi ili kuepuka migogoro ya wafugaji na askari wa wanyama pori pia akasema kua wananchi hawa ndo wanapaswa kua walinzi na watoa taarifa juu ya majangiri ambao wanahujum hifadhi hii maana wao ndo watakao faidika na uwepo wa hifadhi hii kwa asilimia kubwa.Baada ya kusema hayo aliagiza mtuhumiwa huyu kufika ofisi za mhifadhi wanyama pori mjini kondoa siku ya jumanne ya tarehe 17 aprili 2018, na kuagiza taratibu za kisheria zifate mkondo wake ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani huyu alievunja sheria pia hata wale ambao hawajafika kutambua mifugo yao bila kufanya hivyo mifugo yao itapigwa mnada na serikali baadaya siku thelathini (30).
Utaratibu unaopaswa kufuatwa mara inapobainika kupotea kwa mifugo imeelezwa kua mwananchi anapaswa kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji chake pili kwa mtendaji wa kijiji ili mtendaji afanye utaratibu wa kuwasiliana na meneja wa hifadhi ili apewe kibari cha kuingia hifadhini kutambua mifugo yake na kuepuka kuingia hifadhini bila kibali.Ikumbukwe kua upewapo kibali kutambua mifugo yako siyo kigezo cha kuchukua mifugo la hasha utambuzi utafanyika kisha sheria itafuata mkondo wake kama sheria za hifadhi zinavyosema alisema Naibu waziri
. Katika picha ni miongoni mwa ng'ombe 1298 wanaoshikiliwa ndani ya hifadhi ya mkungunero, kwa wale wote waliopotelewa mifugo yao wanaagizwa kuwasiliana na meneja wa hifadhi kwa ajili ya utambuzi wa mifugo yao ili kuepuka mifugo yao kupigwa mnada. Katika picha ni Mhe, naibu waziri Japhet Hasunga akimsikiliza mmoja wa walalamikaji . Picha na mwandishi wetu.
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,KILIMANI STREET
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.