Mhe. Rais Dkt. Magufuli amefungua barabara ya kiwango cha lami ya Dodoma-Babati (Km-251) leo tarehe 27/04/2018.Barabara
hii iliyogharimu jumla ya Sh. bilioni 378.423 imejengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benki
ya Maendeleo ya Afrika na Serikali ya Japan.Rais amesema barabara hiyo ni sehemu ya Barabara Kuu ya kaskazini inayoanzia
Cape Town hadi Cairo yenye jumla ya km 10,288 itakayounganisha Kusini na Kaskazini mwa bara la Afrika ikipita nchi nane.Rais
Dkt. Magufuli amewataka wananchi wa Kondoa, vyombo vya Usalama barabarani na madereva wa vyombo vya moto wazingatie
matumizi bora ya barabara ili kuepuka ajali, kuzingatia sheria za barabarani na kusimamia maadili ya udereva ili kupunguza vilio
vya watu kutokana na ajali.Mhe. Rais aliendelea kusisitiza kuwa Kukamilika kwa barabara hii ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya
CCM.
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,KILIMANI STREET
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.